Bendi ya Msondo Ngoma Music Band imeandaa onyesho maalum kwa ajili ya kumtambulisha wamamuziki wake mpya Shaban Dede, linatlotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo jijini Dar es salaam jumapili Mei 8.

Onyesho hilo litasindikizwa na kundi la muziki wa taarabu la Coast Modern Taarab linaloongozwa na mwimbaji Omary Tego, mmoja wa waratibu wa onyesho hilo amesema litaaza muda wa saa kumi na mbili jioni huku kukiwa na burudani nyingine mbalimbali.

Kiingilio katika onyesho hilo kitakuwa ni shilingi 5,000 ambapo mwanamuziki Shaban Dede amesema, anatarajia kuwa onyeshpo litakuwa ni zuri na mashabiki wa bendi ya Msondo Ngoma na muziki kwa ujumla wake watafurahia.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: