Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akizingumza katika hafla ya kuwaaga wakufunzi 25 wa VETA kwenda Nchini Finland kujifunza ujuzi wa Teknolojia zinazohitajika katika uchimbaji na ukuzaji mnyororo wa thamani wa Madini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Serikali imeendelea kuimarisha juhudi za kukuza ujuzi wa kisasa katika sekta ya madini baada ya wakufunzi 25 kutoka VETA kuagwa rasmi kuelekea nchini Finland kwa ajili ya mafunzo maalumu ya ufundi stadi katika sekta hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wakufunzi hao, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, alisema mpango huo unalenga kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi wa kisasa watakaosaidia kuinua sekta ya madini na kutoa fursa zaidi za ajira kwa vijana nchini.
Alisisitiza kuwa wakufunzi hao wanapaswa kutumia ipasavyo fursa hiyo ili kurejea na maarifa mapya yatakayosaidia kuboresha shughuli za uchimbaji, kuongeza thamani ya madini na kuimarisha ushindani wa bidhaa za madini za Tanzania katika soko la kimataifa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Anthony Kasore, alisema mafunzo hayo ni sehemu ya mradi wa kimkakati unaotarajiwa kuwafikia zaidi ya Watanzania 400, hususan wanaojihusisha na uchimbaji madini, huku ukitoa kipaumbele kwa wanawake na makundi maalum.

Naye Katibu Mtendaji wa NACTVET, Mwajuma Lingwanda, alisema mradi huo utaongeza ubora wa mafunzo ya ufundi stadi na kusaidia kuzalisha wataalamu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Baadhi ya matukio katika hafla ya kuwaaga wakufunzi 25 wa VETA kwenda Nchini Finland kujifunza ujuzi wa Teknolojia zinazohitajika katika uchimbaji na ukuzaji mnyororo wa thamani wa Madini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
---
Aidha, mwakilishi wa Wizara ya Madini, Zephaniah Henry, alibainisha kuwa bado kuna upungufu wa wataalamu katika sekta ya uchimbaji madini, hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuziba pengo hilo kwa kuongeza wataalamu wenye ujuzi wa kisasa.

Wakufunzi hao wanatarajiwa kupata mafunzo katika maeneo mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa kisasa wa madini (digital mining), usalama na afya migodini, utunzaji wa mazingira pamoja na matumizi ya mitambo ya kisasa.
Akizungumza kwa niaba ya wakufunzi, Neema Lyimo kutoka VETA Dodoma alisema wamejipanga kuhakikisha ujuzi watakaoupata unasaidia kuimarisha sekta ya madini na kuwainua vijana kiuchumi kupitia ajira na ujasiriamali.
Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akiwa katika ya pamoja na wakufunzi 25 wa VETA wanaoenda Nchini Finland kujifunza ujuzi wa Teknolojia zinazohitajika katika uchimbaji na ukuzaji mnyororo wa thamani wa Madini iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: