Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania PLC, Chiha Nchimbi (wa pili kushoto), akikabidhi kapu la zawadi kwa Rehema Sangaya, mkazi wa Hombolo, Dodoma (wa tatu kushoto), ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za msimu wa Sikukuu. Tukio hilo limefanyika jijini Dodoma jana, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Vodacom kurejesha kwa jamii na kusherehekea wateja katika kipindi hiki cha sikukuu.Wanaoshuhudia tukio hilo ni pamoja na Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wilayani Kondoa Balikulije Mchome, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoyo Julius Magawa (wa pili kulia) na Mtendaji wa Mtaa wa Mkoyo, Pendo Mwijalubi (kushoto).





Toa Maoni Yako:
0 comments: