Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema kuwa wataendelea kuipa ushirikiano i Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ili kukuza biashara nchini.

Hata hivyo ameipongeza TanTrade kwa utendaji wake katika kuendeleza masoko ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi kupitia maonesho ya biashara na misafara ya kibiashara ya kimataifa.

Waziri Kapinga ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi alitembelea ofisi za TanTrade zilizopo jijini Dar es Salaam.

Amesema taasisi hiyo ina mchango mkubwa katika kuwaunganisha wazalishaji wa Tanzania na masoko ya kikanda na kimataifa.

Amesema kuwa jitihada za TanTrade zimeongeza fursa kwa wafanyabiashara, kuchochea kuongezwa kwa thamani ya bidhaa, na kuimarisha utambulisho wa bidhaa za Tanzania nje ya nchi.

Waziri Kapinga pia aliiagiza mamlaka kuhakikisha wanaboresha mifumo ya kidijitali kuweza kusomana na mifumo mingine ili kurahisisha kwenye upatikanaji wa taarifa za biashara na masoko kwa wadau.

Alisisitiza kuwa upatikanaji wa takwimu sahihi na kwa wakati ni muhimu katika kusaidia maamuzi ya kibiashara na kuongeza ushindani wa nchi katika masoko ya kimataifa.

Aidha, alisema kuwa mfumo mzuri wa utoaji wa taarifa utaharakisha ukuaji wa sekta ya biashara na kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na fursa pana za masoko.

Kwa upende wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Dkt.Latifa Khamis ameaema kuwa ziara ya Waziri wa Viwanda na Biashara wanaenda kufanyia kazi pamoja na kuangali sheria iliyoanzisha Mamlaka hiyo.

Amesema kuwa wamejipanga kufika katika mipaka yote katika kusimamia biashara kubwa ziweze kuendelea kukua na kuleta maendeleo nchini.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: