Na Mwandishi Wetu – Dar es Salaam

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa maelekezo ya kisheria yatakayozingatiwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa masharti ya Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2024.

Taarifa iliyotolewa Oktoba 23, 2025 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima R. K., imefafanua utaratibu utakaotumika kwa wapiga kura katika vituo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mpiga kura hatapewa ruhusa ya kupiga kura endapo:

Kadi yake haina picha lakini taarifa zake binafsi hazipo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Namba ya mpiga kura inatofautiana na ile iliyo kwenye Daftari la Kudumu, licha ya taarifa nyingine kufanana.

Ameandikishwa lakini amepoteza kadi yake au imeharibika, isipokuwa atumie kitambulisho cha Taifa (NIDA), leseni ya udereva au pasi ya kusafiria.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa wapiga kura ambao kadi zao hazipo katika daftari hawataruhusiwa kupiga kura, na wale kutoka katika kata 10 zilizofutwa ikiwemo Kanoge, Litapunga, Katumba, Mtapenda (Ikolongo na Ndurumo) na nyingine zilizoko katika majimbo ya Nsimbo, Tanganyika na Ulyankulu, hawataruhusiwa kupiga kura katika vituo vya zamani.

Tume imesisitiza kuwa lengo la maelekezo haya ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi, uadilifu na kufuata matakwa ya sheria, sambamba na kuwataka wananchi kufuatilia taarifa rasmi za uchaguzi kupitia vyanzo vya Tume.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: