Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) – Mwanza, aliyeripotiwa kupotea tangu Oktoba 9, 2025.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Marco G. Chilya, amesema Padre Nikata alipatikana akiwa hai katika mashamba ya Kijiji cha Mawa, Kata ya Hanga, Wilaya ya Namtumbo, nyumbani kwake.

Alikutwa na begi dogo la mgongoni lililokuwa na taulo, hati ya kusafiria, karanga, fedha taslimu shilingi 13,500, funguo, saa, simu, na dawa alizokuwa akitumia kwa ajili ya maradhi ya ugonjwa wa moyo.

Kwa sasa, Padre Nikata amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songea (Homso) akiendelea na matibabu kutokana na kudhoofika kwa afya yake. Polisi wamesema hakuna ushahidi unaoonyesha chombo chochote cha usalama kilihusika katika tukio la kutoonekana kwake ambalo kwa uchunguzi wa awali linahusishwa zaidi na changamoto za kiafya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: