Mgombea wa kiti cha Ubunge kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Silvestry Koka amerudisha fomu ya kuwania kiti cha Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini Mkoani Pwani leo tarehe 27 Agosti, 2025.

Koka akizungumza na wananchi mara baada ya kurudisha fomu yake katika ofisi za Tume ya Uchaguzi zilizopo Manispaa ya Kibaha amesema kuwa "fomu zimepolewa na kwa sasa najipanga kwa uchaguzi ujao wa 2025" amesema.

"Sasa najipanga kwa kampeni za uchaguzi nawasisitiza kama jinsi tulivyoongea siku nilipochukua fomu kwamba kule tulikotoka tulikua tunafanya mazoezi ya kukimbia na kumpata mkimbiaji bora ambaye ni mimi hivyo tofauti na makundi yafe chama kwanza mtu baadaye"amesema Koka.

"Tofauti zetu tumezimaliza makundi yasiwepo tena kundi ni moja tu ambalo ni CCM, tuungane kwa pamoja tukazitafute kura za wananchi popote walipo ili Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba 29 ,2025" amesema.

Mbunge Koka amesema wananchi Jimbo la Kibaha wahakikishe wamamchagua mkimbiaji namba moja Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge na Madiwani wote wa Kata 14 wanapata kura za kutosha ili kutumiza mafiga matatu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: