Na Oscar Assenga, TANGA

KATIBU MKUU wa Chama cha NLD Doyo Hassan Doyo amesema tayari wamefungua pazia la mchakato wa kuwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho kwa ajili ya kuwapata wagombea kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025

Doyo aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wanachama wa chama hicho mkoani Tanga ambapo alisema mchakato huo ni kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali zikiwemo za Juu kabisa katika Taifa katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Alisema wameamua kuanz mchakato huo mapema ili kuweza kuwapata wagombea makini, waledi na wenye sifa ambao watakiwakilisha chama hicho katika uchaguzi huo.

Aidha Katibu huyo aliwataka wagombea wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbali mbali na hawatatoa ada za fomu ili kuwapa nafasi kubwa ya kuwa wagombea katika Uchaguzi huu wa mwaka 2025.


“Hii ni kuondoa dhana ya kumnyima mwanamke fursa ya kugombea nafasi ndani ya Chama na kushindwa kumudu gharama hizo fedha hivyo tumewaondolea adha za fomu “Alisema Katibu huyo.

Doyo alisema kwamba maamuzi ya kutangaza pazia hilo yanatokana na kikao cha Kamati Kuu wa chama hicho iliyofanyika February 23 mwaka huu ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wao wa Taifa Mfaume Hamsi Hassani.

Alisema katika kikao hichp miongoni mwa mambo yaliyozungumza ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na wamekubaliana na kamati kuu imeagiza sekretarieti itoe taarifa rasmi kuhusu mchakato huo.


Kuhusu wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar watajulikana katika mkutano mkuu wa chama hicho utakaofanyika mwezi Aprili mwaka huu ambao utawapitisha pia wagombea.
Hata hivyo alisema zoezi la kuchukua fomu na kurudisha kwa upande wa udiwani na ubunge limeanza tokea Machi 1 mwaka huu ambalo litakwenda hati Julai 31 mwaka hu
“Natangaza rasmi kwamba chama kimefungua pazia la kwania nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na za Uraisi fomu zimeanza kutoka 26 mwezi wa pili “Alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: