Na Oscar Assenga, TANGA.
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imesema kwamba inaendelea na mikakati ya kuboresha miundombinu ya Mapango ya Amboni yaliyopo Jijini Tanga ili yaendelee kuwavutia watalii wengi zaidi.
Hayo yalibainishwa February 14 mwaka huu na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko NCAA Mariam Kobelo wakati wa kampeni ya kuhamasisha utalii wa ndani katika eneo la Mapango hayo kampeni hiyo iliambatana na Mashindano ya Mapishi.
Alisema kwa sasa wana mpango wa utekelezaji wa mikakati ya kuboresha miundombinu ikiwemo mfumo wa ukusanyaji wa mapato,kujenga maeneo ya kupumzikia pamoja na uwekwaji wa kambi za wageni ambao wanakwenda kutalii na kupenda kulala hapo hapo.
“Labda niwaambie kwamba kuhitimishwa kwa kampeni hii leo itatusaidia kufungua fursa ya kuongeza kipato kwa wajasiriamali wadogo wa ndani ya wilaya ya Tanga “Alisema Mariam.
Awali akizungumza Mkuu wa wilaya ya Tanga Japhari Kubecha aliupongeza uongozi wa NCAA kwa kuja na ubunifu ambao kupitia kampeni hiyo imeongeza hamasa kubwa ya utalii wa ndani katika mkoa huo na hivyo kukuza utalii.
Mkuu huyo wa wilaya aliwahaidi mamlaka hiyo kwamba Serikali ya wilaya hiyo itaendelea kushirikiana nao kuendeleza na kutunza mapango hayo ya pekee .
“Lakini niwapongeze uongozi wa NCAA kwa kuweza kuinua hadhi ya Mapango ya Amboni ambayo ni kuvutia kikubwa kwa watalii kutoka nje na ndani kutembelea hivyo kutokana na hamasa hii tutaweza kuongeza pato la nchini”Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: