Wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa wakionyesha silaha ya khanga yenye ujumbe wa kupinga vitendo hivyo uliyotumika kufikisha mawasiliano kwenye jamii wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyomalizika mwishoni mwa wiki
Baadhi ya Wanawake wa Kakola wilayani Kahama wakifuatilia mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wakiwa wamevaa Khanga zenye ujumbe wa kupinga vitendo hivyo.


Baadhi ya Wanawake wa Kakola wilayani Kahama wakifuatilia mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wakiwa wamevaa Khanga zenye ujumbe wa kupinga vitendo hivyo.

Na Mwandishi Wetu.

Vazi la utamaduni la khanga ambalo asili yake ni Afrika Mashariki limeanza kutumika miaka mingi iliyopita katika makundi mbalimbali ya jamii ambapo hadi leo ni vazi ambalo pamoja na mabadiliko ya mitindo ya mavazi ambayo hubadilika kila mara limeendelea kuwa na hadhi yake.

Khanga ni vazi lenye mvuto na linaweza kutumika kwenye sanaa, utamaduni, michezo na shughuli mbalimbali hata za kitaifa na baada ya kuwekewa maneno ya nakshi ili kuweza kufikisha ujumbe husika.

Watafiti wanabainisha kuwa Vazi la khanga ambalo asili yake ni Zanzibar, lilianzishwa kutokana na ushawishi wa wareno, ambapo khanga ya kwanza kuchapishwa ilikuwa yenye rangi nyeusi na nyeupe mwaka 1860.

“Khanga inavaliwa na wakinamama, watoto na wanaume wakiwa majumbani, kwenye sharehe kwenye matukio mbalimbali ya utamaduni na ngoma, jikoni wakati kuandaa chakula,kwenye ibada na limekuwa maarufu sana Afrika Mashariki na baadhi ya maeneo ya Afrika ya Kati hasa katika maeneo ya Pwani kama Dar es Salaam, Mombasa na Zanzibar.

Umaarufu wa vazi hili umekuwa sio wa rangi au maua yake bali maneno yanayokuwa kwenye vazi hili ambayo hufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa walengwa haraka zaidi.

Kwa miaka mingi vazi hili limekuwa likitumika kutoa ujumbe wa kuonya, kufundisha, kushawishi na kuburudisha kwenye jamii pia kwenye matukio ya ibada na mawasiliano ya kutumia khanga yamekuwa yakiwafikia walengwa haraka.Vazi hili pia limekuwa likitumika kwenye kampeni mbalimbali zikiwemo za kisiasa na afya.

Mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia moja ya kivutio kikubwa lilikuwa ni matumizi ya khanga zenye ujumbe wa kupinga vitendo hivi ambazo ziligawiwa kwa Wanawake sehemu mbalimbali vijijini na kuvaliwa na Wanawake kila walipoenda kwenye mikusanyiko ya kuapata mafunzo na katika shughuli zao za maisha ya kila siku.

Akiongelea nguvu ya matumizi ya khanga katika kampeni kama hizi Mratibu wa Dawati la Kijinsia Taifa kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, ACP Faidha Suleiman, alisema kwamba vazi la khanga limeweza kufikisha ujumbe kwa wakinamama hasa wale ambao wako maeneo ya vijijini ambako hakuna vyanzo vingi vya kupata taarifa.

Naye Meneja Uhusiano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa akieleza umuhimu wa khanga kama chombo cha mawasiliano alisema khanga kwa miaka mingi imekuwa ni nyenzo ya kufikisha ujumbe kwa walengwa na ndio sababu katika mwaka huu wadau katika kupinga ukatili wa kijinsia waliamua kuwapatia wanawake katika maadhimisho hayo ili kuweza kuongeza msukumo wa uelewa wa mambo ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kukabiliana nayo kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

Pamoja na mambo mengine kuhusu tukio hilo ila sifa nyingine ya vazi la Khanga inaaminika kuwa ni vazi la siri pia kwa kuwa linahusisha mahusiano ya mapenzi ndio maana wanaume huwa hawawezi kuvaa vazi hilo hadharani.

Pamoja na umaarufu mkubwa wa vazi hilo kutumika katika ukanda wa pwani ,Khanga inachapishwa katika nchi za bara la Asia kama India na China, wabunifu na waandishi wa khanga hizo bado wana changamoto ya kuendelea kuandika maneno ambayo yanaweza kuleta matokeo chanya kwenye jamii kwa mfano kuwa na ujumbe wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Wadau ambao wanabuni khanga zenye ujumbe maridhawa kwa jamii hawana budi kupongezwa kwa kuwa wabunifu wengi wa Khanga wako kibiashara zaidi ambapo mara nyingi wanabuni ujumbe wenye masuala ya mapenzi zaidi kuliko ya kubadilisha jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: