Wanufaika wa miradi inayofadhiliwa na TNRF, GEF SGP kupitia UNDP Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandaaji wa taarifa na kujengewa uwezo wa utekelezaji wa miradi.
Connecting Youth Connecting Tanzania (CYCT) imeshiriki kikamilifu katika warsha ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza miradi na kuandaa ripoti za maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na Mpango wa Ruzuku Ndogo wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF SGP) kupitia UNDP Tanzania. Warsha hii imefanyika tarehe 19 hadi 20 Septemba 2024, jijini Dodoma, ikiwaleta pamoja wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kiraia na sekta binafsi.
Katika warsha hii, mwakilishi wa CYCT amejifunza mbinu bora za utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha hali ya mazingira, pamoja na njia sahihi za kuandaa na kuwasilisha ripoti za kiufundi na kifedha. Mafunzo haya yalijumuisha usimamizi wa muda, matumizi bora ya rasilimali, ushirikishaji wa jamii, pamoja na jinsi ya kuhakikisha mradi unafikia malengo yaliyokusudiwa.
Kupitia ushiriki huu, CYCT imepata uelewa wa kina wa viwango na taratibu zinazohitajika katika kuwasilisha taarifa za maendeleo ya mradi kwa wakati. Hii itasaidia katika utekelezaji wa mradi wa kurejesha na kulinda misitu ya West & North Kilimanjaro, ambao unalenga kuboresha hali ya mazingira na kujenga uhimili wa mabadiliko ya tabianchi kwa jamii zinazozunguka hifadhi hiyo.

CYCT inaamini kuwa mafunzo haya yataboresha uwezo wake wa kusimamia miradi kwa ufanisi zaidi, na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha malengo ya mradi kwa manufaa ya mazingira na jamii kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: