Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K akizungumza wakati wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K akizungumza wakati wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K akizungumza wakati wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele (katikati), Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima R. K (kulia) na Mkurugenzi Ofisi ya Zanzibar, Bw. Adam Mkina (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na washiriki wa mafunzo ya watendaji wa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
************
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka watendaji wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kwahani, Zanzibar kutekeleza wajibu na majukumu waliyopewa kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni na miongozo iliyotolewa na itakayotolewa na Tume wakati huu wa uchaguzi mdogo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Jacobs Mwambegele wakati wa akifungua mafunzo kwa mratibu wa uchaguzi, msimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo yanayofanyika kuanzia leo tarehe 13 hadi 15 Mei, 2024 Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Alisema uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo ndio msingi wa uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza au kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
“Nachukua nafasi hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi, mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea. Hivyo, itafaa zaidi tutakapohitimisha mafunzo yetu hapa, sote tuwe na utimamu wa kusimamia uchaguzi kwa ufanisi wa hali ya juu badala ya uzoefu.”, alisema Mhe. Jaji (R) Mwambegele.
Mbali na kuzingatia sheria, Mhe. Jaji (R) Mwambegele aliwakumbusha washiriki wa mafunzo na kuwasisitiza kuwa, wakati wote wa mchakato wa uchaguzi, ni vema wakavishirikisha kwa karibu vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi kuhusu masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia utekelezaji wa majukumu wao.
Aliongeza kuwa ni muhimu kwa watendaji hao wa uchaguzi pia, kuhakikisha wanalitambua na kulijua vyema eneo ambalo uchaguzi utaendeshwa ikiwemo miundombinu ya kufika katika vituo vya kupigia kura.
Pamoja na mambo hayo, Mhe. Jaji (R) Mwambegele aliwasisitiza kufanya utambuzi na kukagua vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum ya vituo husika kwa lengo la kuhakikisha mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani.
“Kuhakikisha mnaajiri watendaji wa vituo wenye weledi, wanaojitambua na tuachane na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za uchaguzi”, alisema Mhe. Jaji (R) Mwambegele na kuongeza kuwa:
“Kuhakiki vifaa vya uchaguzi mnavyopokea kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema; kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala.
“Kuhakikisha siku ya uchaguzi mnaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi; na kufanya mawasiliano na Tume pale ambapo utahitajika ushauri kuhusiana na masuala ya uchaguzi.”
Mhe. Jaji (R) Mwambegele aliwakumbusha watendaji hao kuwa wameaminiwa na kuteuliwa kwa sababu wanao uwezo wa kufanya kazi ya kusimamia uchaguzi, hivyo jambo muhimu mnalotakiwa kuzingatia ni kujiamini na kufanya kazi kwa weledi na kwamba.
Aliwataka kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria ya Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na yatakayotolewa na Tume katika kipindi hiki cha uchaguzi mdogo.
Mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi yemelenga kuwakumbusha mambo muhimu kuhusu usimamizi, uratibu na uendeshaji wa uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kwahani lililopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.
Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, fomu za uteuzi wa wagombea zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 17 hadi 23 Mei, 2024, siku ya uteizi ni tareghe 23 Mei, 2024 wakati kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 18 Mei hadi Juni 7, 2024 na siku ya uchaguzi itakuwa tarehe 08 Juni, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments: