NA WILLIUM PAUL.

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ikiongizwa na Mwenyekiti wake Mohammed Ali Kawaida (MCC) wamekabidhi msaada wa Chakula kwa wananchi wa Rufiji walioathirika na mafuriko katika maeneo hayo.

Kawaida ameelekeza Viongozi wa Rufiji kuhakikisha misaada yote inayotolewa inawafikia wananchi hao waliothirika na Mafuriko

"Niwasihi sana viongozi hakikisheni misaada hii inawafikia walengwa ambao ni wananchi wenzetu walioathirika na mafuriko na tuendelee kuwa faraja kwa ndugu zetu" Alisema Kawaida
Aidha Kawaida amewahakikishia wananchi wa Rufiji kuwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi itaendelea kuwa karibu nao katika kipindi hiki kigumu wanachopitia kwani ni Utamaduni wa UVCCM kuwakimbilia Wananchi pale wanapopatwa na Matatizo.

"Ndugu zangu sisi Jumuiya ya Vijana tuna utamaduni wetu wa kuishi kama ndugu wamoja ndio maana kauli Mbiu yetu ni "Kulinda na Kujenga Ujamaa", Hivyo niwahakikishie kuwa tutaendelea kuwa karibu na ninyi katika kipindi hiki kigumu"

Kawaida amewasihi Watanzania na Wadau mbalimbali wawakimbilie Wananchi wa Rufiji kuwasaidia wananchi wa Rufiji na sio kufanya Siasa.




Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: