MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akiwa kwenye futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) na Waziri wa Maji.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso akitunzwa baada ya kusoma Quarn Tukufu katika halfa hiyo.
Na Oscar Assenga, PANGANI.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt Samia Suluhu mkoa huo umepokea fedha kiasi cha Sh.Trilioni 2.6 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Balozi Batilda aliyasema hayo wakati wa Dua Maalumu ya Kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu iliyokwenda sambamba na Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) na Waziri wa Maji Jumaa Aweso iliyofanyika wilayani Pangani.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Serikali,Chama na Taasisi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa maji Mhandisi Mathew Kundo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji,Mkurugenzi wa Ruwasa na wataalamu mwengine.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema fedha hizo zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo likiwemo Daraja la Mto Pangani na Barabara ya Pangani pamoja na mengine ikiwemo ya elimu ambapo wanamshukuru Rais kwa ujenzi wa mabweni ya watoto wenye mahitaji maalumu yamejengwa, zahanati, nyumba za walimu na miradi ipo mingi kazi kubwa imefanywa.
“Katika hili tunamshukuru sana Mh Rais Dkt Samia Suluhu kwa kutuletea fedha hizi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo lakini namshukuru kwa imani kubwa kwangu ninahaidi sitamuangusha nitajitahidi kwa ushirikiano wenu na dua zengu niweze kutimiza yale ambayo anakusudia nitimize nikiwa hapa Tanga” Alisema RC Balozi Batilda.
Alisema kwamba wataendelea kuhakkikisha fedha zinazokuja zinatekeleza kazi iliyokusudiwa na sio vyenginevyo pamoja na usimamizi mzuri katika miradi inayotekeleza ili iweze kuleta tija inayotakiwa.
“Nimshukuru Waziri Aweso amefanya jambo kubwa na ameendelea kufanya mambo mengi kwenye Sekta ya Maji nimetoka Tabora kwenye miradi 28 nasi tulikuwa tunanufaika nimekuja hapa Tanga nimeambiwa napo ipo ni kijana mdogo lakini mwenye hekima, hofu ya mungu, mchapakazi “Alisema RC Balozi Batilda.
Alisema kwa hakika dhamana aliyopewa na Rais Dkt Samia Suluhu kuhakikisha anawatua wakina mama ndoo kichwani ameitekeleza vizuri kwa kushirikiana na wataalamu wa wizara maji wanaendelea na kazi nzuri.
Akizungumzia suala la mabadiliko ya tabia ya nchi hasa kwenye wilaya ya Pangani RC Balozi Batilda alisema wilaya hiyo ni moja ya maeneo yaliyoathirika na kuna maeneo yakichimbwa visima kuna maji ya chumvi ndio maana kwenye mradi wa maji ya miji 28 na wao wamepelekewa na maeneo watachimba visima ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata maji safi na salama.
Akizungumzia suala la uvuvi RC huyo alisema suala hilo katika mkoa huo ni moja ya maeneo ya uvuvi hivyo suala la maboti na vifaa vya uvuvi vitaendelea kupatikana kwenye mji wa Pangani na maeneo mengine.
“Tunapozungumzia masuala ya mazingira niwape kongole Pangani mazingira mmeendelea kuyatuza na msitu wenu wa asili unapendeleza”Alisema
Mkuu huyo wa mkoa alisema katika moja ya kuendeleza ukwekezaji Serikali kupitia Wizara Madini ilisaini mkataba na wawekezaji wa madini ya Ndovu au tembo ambayo yatachimbwa kwenye Mwambao wa Pangani karibu kilomita 15 ya ufukwe.
Alisema walichowaambia wahakikisha hawawanyi ruhusu ya wavuvi kutumia mwambao huo na matumbawe hayatavurugwa ikiwemo mikoko iliyopo wakati wanaendelea kunufaika na mradi huo na kuendelea na uvuvi,matango pori yote kuhakikisha wanakuwa na shughuli mbalimbali zinaendelea.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa wa Tanga ndio ambao kila kitu kinaweza kuota hivyo lazima wahakikishe utajiri huo unawanufaisha wananchi wao wote kwa kuhakikisha wanachangamkia fursa zilizopo.
“Katika ujenzi wa bomba la mafuta litapita kwenye wilaya kadhaa tunataka wana tanga wanufaike na miradi hiyo na kazi yake katiba tawala na wakuu wa wilaya na makatibu tawala ni kuwawezesha wananchu kuona fursa za uwepo wa mradi huo ili waweze kuchangamkia fursa hizo”Alisema RC Balozi Batilda ,
Awali akizungumza katika futari hiyo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew alisema kwamba maadili mema ambayo tumeyaonyesha katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani tuendelee kuifanya na kufanya ibada ndio tunaweza kuwaponya wengi na kujiponya na sisi.
Mhandisi Mathew alisema pia waendelee kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu ili aendelea kuifanya kazi nzuri anaoendelea kuifanya na kuhakikisha wanashirikiana na Mbunge wao na kamwe wasimwangushe .
“Nataka kuwaambie wana Pangani “Dhahabu ya Pangani tunaijua wana Pangani na Dhahabu ya Tanzania tunaijua na tusije kudanganyika na kuachia dharabu hii na kwenda kuokota mawe”Alisema
Hata hivyo alimshukuru Waziri Aweso kwa jambo kubwa alilolifanya kwa wananchi wake kutokana na uwepo wa umoja na mshikamano kwa wananchi wake ambao wameitika kwa wingi kwenye tukio hilo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman alisema safari ya kuifungua pangani kimaendeleo itafanywa na wana Pangani wenyewe na mimi ni miongoni mwa watu walishawishika na Waziri Aweso kipindi kile kwa maneno yake kwa dhamira iliyojificha ndani ya moyo wake akanitamkia ya kutaka kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo.
Alisema kwa sasa tunayaona maendeleo makubwa sana kwenye Jimbo la Pangani ikiwemo ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani –Saadani ambayo itaifungua wilaya hiyo pamoja na uwepo wa miradi ya maji ambayo awali wananchi walikuwa wakiifuata umbali mrefu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: