MRADI wa kuangalia namna bora ya kutumia maduka ya dawa katika kutoa dawa za kujikinga na maambukizi ya Ukimwi hasa kwa vijana hasa wa kike utakwenda kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo kwa vijana hao.
Akizungumza wakati wa kikao cha wadau kutambulisha mradi huo, Msimamizi Kiongozi wa Mradi na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Dk.mackfallen Anasel amesema mradi huo utafanyika katika mikoa ya Shinyanga, Kagera na Geita.
Amefafanua katika kutekeleza Mradi huo Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na Wizara ya Afya wanashirikiana na Chuo Kikuu cha California San Francisco(UCSF)Chuo Kikuu cha California Berkeley( UCB) na Shirika la H-PON.
Ameongeza kwamba mradi huo unalenga kuangalia namna bora ya kuyatumia maduka ya dawa kutoa dawa za kujikinga na maambukizi ya Ukimwi ambapo wamelenga watoto wa kike.
"Kulingana na tamaduni namna huduma zinavyotolewa katika vituo vyetu vya afya watoto wa kike wamekuwa wakikumbana na unyanyapaa au kuona aibu kwenda kuchukua dawa hizi kwa ajili ya kujikinga kupata hivi virusi.
"Mradi huu utakuwa ni wa miaka mitano na tutakuwa tunatafuta namna gani bora ya kutumia haya maduka ya dawa kutoa hizi huduma kwa ushirikiano wa haya mashirika niliyoyataja pia kutatengenezwa program itakayowajengea uwezo watalaam katika ngazi ya wilaya na ngazi ya mkoa."
Ameongeza pia kufanya tafiti ambazo zinatokana na wao walivyofanya tafiti mbalimbali ili mwisho wa siku kupata tafiti zitakazosaidia kuboresha sera na miongozo mbalimbali.
"Hivyo tuweze kuwa na miongozo inayotokana na tafiti za ndani ambazo zinaweza kutufanya tuboreshe na kukabiliana na janga la UKIMWI."
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Geita Dk.Omar Sukari amesema katika kikao hicho wamepata nafasi ya kushiriki kwenye kikao cha utambulisho wa mradi ambao unalenga vijana wa kike..
"Kimsingi ni mradi ambao unajielekeza kutanua huduma kuhusu upatikanaji wa dawa za kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana hasa katika mikoa mitatu ambapo mradi unakwenda kutekelezwa.
"Tumefurahi kama waganga wakuu wa mikoa kushiriki kwenye mradi unaokwenda kutekelezwa katika mikoa yetu.
"Ni mradi wa ubunifu ambao unatoa nafasi kwa vijana wa kike ambao wako kwenye rika balehe na wale ambao tayari wameshakuwa vijana wenye umri miaka 28 ili kupata uwezo kuzikifia huduma za kupata dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya UKIMWI, " amesema.
Ameongeza wanajua vijana ni kundi ambalo kwa namna moja au nyingine ndilo hatarishi na asilimia 25 ya maambukizi kwa vijana yako katika kundi hilo.
Hivyo kundi hilo wakilifanyia ubunifu wa kupata dawa hizo kupitia kwenye maduka ya dawa inawezekana kuongeza uwezo wa huduma ambazo watakuwa wanazitoa kupitia maduka hayo.
"Kwa hiyo sisi kama waganga wakuu wa mikoa tunaona ni ubunifu mzuri na utakapokamilika utasaidia Wizara na wadau kutengeneza miongozo ,sera nzuri ya afya namna ya kuwafikia vijana na makundi mengine ambayo yapo kwenye hali hatarishi.
"Kwa hiyo tunadhani ni kitu kizuri, vijana wanakuwa na uhakika wa kupata huduma na itawapa nafasi kwa namna gani waweze kupata huduma."
Kwa upande wake Dk.Eno Machangu amesema mradi huo umelenga kuwafikia vijana na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hususani kwa ajili ya vijana rika balehe, vijana wa kike rika balehe kwa lengo la kuwasaidia kupata huduma zaidi za afya lakini kujikinga zaidi na maambukizi ya
Toa Maoni Yako:
0 comments: