Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN) leo umefanya mkutano usio rasmi na chakula cha mchana na Bi. Jeanne Clark Afisa wa Masuala ya Umma na Kalisha Holmes Afisa Habari kutoka Ubalozi wa Marekani kwa mtiririko huo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho wanachama waandamizi wa TBN waliohudhuria walijadili mambo kadhaa na maofisa hao ikiwemo mipango ya sasa na ya baadaye ya chama.

"Tulishiriki kwa kutoa maoni yetu ya namna kukiendeleza zaidi chama ili kukuza kazi muhimu inayofanywa na wanachama wetu tangu kuanzishwa kwake mapema 2015," mmoja wa wanachama mwanzilishi wa TBN Josephat Lukaza alisema.

"Tulifurahishwa kujua kwamba Ubalozi wa Marekani inafuatilia kwa karibu kazi za waandishi wa habari mtandaoni na kuonesha nia ya kushirikiana na TBN", alisema John Bukuku, mwanablogu mwingine mkongwe.

Wajumbe hao wa TBN waliushukuru Ubalozi wa Marekani kwa kuonyesha nia ya kutoa fursa za mafunzo ili kuimarisha taaluma na kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, wakisema kuwa hatua hiyo inatia moyo kwa kweli.

Mwanablogu mwanzilishi Muhidin Issa Michuzi alisema kuwa ushirikiano baina ya TBN na watu kama ubalozi wa Marekani unaolenga mafunzo ya weledi wa uandishi na kuzingatia maadili ya taaluma hii utasaidia saną katika kuinua viwango vya uandishi wa habari mtandaoni nchini Tanzania.

"Kujitolea kwa ubalozi wa Marekani kukuza mazingira ya kuunga mkono na kuwawezesha wanablogu na waandishi wa habari mtandaoni ni jambo la kutia moyo. Tuna imani kwamba ushirikiano huu utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji na maendeleo ya chama chetu, pamoja na sura pana ya vyombo vya habari nchini Tanzania",

Michuzi aliongeza: “Tunafurahia kuwepo kwa uwezekano wa ushirikiano na Ubalozi wa Marekani wa siku zijazo na matokeo chanya yatakayotokana na Ushirika huo utanufaisha wanachama wetu na jumuiya ya wanablogu wa Tanzania kwa ujumla..”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: