Ujumbe wa Wachimbaji wadogo wazawa wa Madini takribani mia Moja kutoka Nchini Tanzania ambao ni sehemu ya Shirikisho wa Wachimba Madini wadogo Tanzania (FEMATA) umewasili Nchini China kwa ziara Rasmi ya siku sita yenye lengo la kujifunza Teknolojia ya Uchimbaji, kujipatia Uzoefu, kutafuta Wawekezaji na kufungua fursa za Kibiashara ya Madini.

Msafara huo uliiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo pamoja na Rais wa FEMATA umepokelewa Jijini Guangzhou na Konseli Mkuu Ndugu. Khatib Makenga kwa niaba ya Balozi wa Tanzania Nchini China Mhe. Mbelea Kairuki ambaye ni sehemu ukamilishaji wa fursa hiyo ya Wachimba Madini kutembelea maeneo mbalimbali Nchini China inayounganisha Wawekezaji wa Nchi hiyo na Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: