Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amelihutubia Baraza la kazi Duniani yenye makao makuu ya Un, Jijini Geneva nchini Uswisi kuonesha juhudi za nchi ambazo zimefikiwa kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo Sheria za kazi, ajira na jinsi.

Akitoa hotuba yake Juni 12, 2023 nchini humo wakati anahutubia baraza hilo, Profesa Ndalichako ameeleza namna Tanzania inavvyofuata mikataba ya kimataifa kuhusu masuala ya kazi, ajira,hifadhi ya jamii na ushirikishwaji wa sauti za makundi mbali mbali kutoka kwa waajiri na wafanyakazi.

Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanya vizuri katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa kuanzisha sheria inayoruhusu watu walio katika sekta isiyo rasmi kuchangia na kunufaika na mafao ya hifadhi ya jamii.Pia imekua miongoni mwa nchi za mfano katika kutekeleza programu ya mafunzo ya uanagenzi.


Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: