Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof Joseph Ndunguru (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mamlaka hiyo Mkoa wa Shinyanga baada ya kuzungumza na Wafanyakazi wa Mamlaka hiyo katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo mkoani humo. Wa kwanza kutoka kushoto ni Msimamizi wa Kituo cha TPHPA Mkoa wa Shinyanga, Jesca Ndomba, na wa tatu ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza Tumbo
Na Mwandishi, Wetu, Shinyanga
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imesema itaendela kuboresha miundombinu yake na huduma kwa wananchi hili waweze kupata tija katika sekta ya kilimo kama ilivyo dira na dhima ya Wizara ya Kilimo.
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Prof Joseph Ndunguru wakati
akizungumza na wafanyakazi wa mamlaka hiyo Mkoa wa Shinyanga na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na kufuata maadili ya kazi zao.
Prof. Ndunguru amesema Serikali inamategemeo makubwa na mamlaka hiyo katika utatuzi wa changamoto zinazowasumbua wakulima hususan katika udibiti wa wadudu waharibifu wa mazao pamoja na visumbufu .
Akitoa taarifa ya utendaji kazi msimamizi wa kituo cha TPHPA Mkoa wa Shinyanga, Jesca Ndomba amesema wameweza kudhibiti visumbufu katika wilaya za Shinyanga ,mkoa wa Tabora ,Simiyu na Kigoma.
Wafanyakazi wa TPHPA wakichukua wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Prof. Ndunguru.
Wafanyakazi wa TPHPA wakiwa katika picha ya pamoja na Prof. Ndunguru (wa tatu kutoka kushoto)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof Joseph Ndunguru (kulia) na Msimamizi wa Kituo cha TPHPA Mkoa wa Shinyanga, Jesca Ndomba wakipitia taarifa mbalimbali wakati wa mkutano huo na wafanyakazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: