Zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepewa mafunzo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), ili kuwawezesha kufanya tathmini stahiki kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini.
Akifungua mafunzo hayo yanayofanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku tano kuanzia Jumatatu Mei 22, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewataka washiriki kuzingatia elimu watakayoipata.
“Mkahakikishe tathmini zinafanyika kwa usahihi na wafanyakazi watakaopata majanga ya ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wapate fidia stahiki na kwa wakati. Hii itaongeza ari kwa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii wakijua wana uhakika wa kinga ya majanga kazini” amesema Masala.
Masala ambaye amefungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla ameongeza kuwa ni vyema waajiri wakahakikisha wafanyakazi wao wanajiunga na mfuko wa WCF ili kuondolewa mzigo wa gharama za majanga mbalimbali yanayoweza kutokea kazini.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, amesema mafunzo hayo yatawaongezea weledi madaktari hao kufanya tathmini sahihi na kwa wakati hatua itakayosaidia pia wafanyakazi wanaopata majanga kazini kulipwa fidia stahiki na kwa wakati.
Baadhi ya madaktari walioshiriki mafunzo hayo akiwemo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi wamekiri kuwa yatawaongezea ujuzi wa kufanya kazi kwa weledi zaidi na hivyo WCF kulipa fidia stahiki.
Mfuko wa WFC ulianza kutoa huduma kwa wafanyakazi wanaopata majanga kazini mwaka 2016 ikiwa ni mwaka mmoja tangu kuanzishwa, ukichukua nafasi ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo ilionekana kutotoa fidia stahiki kwa wafanyakazi waliopata majanga kazini.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wanaoumia wakiwa kazini.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika jijini Mwanza kuanzia Jumatatu Mei 22, 2023.
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulssalaam Omar akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu WCF.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kutolewa kwa zaidi ya madaktari 100 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa ambayo ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera ili kuwaongezea ujuzi wa kufanya tathmini kwa wafanyakazi wanaoumia kazini (kupata ajali, kuugua ama kufariki wakiwa kazini) ili kupata fidia stahiki na kwa wakati kutoka WCF.
Madaktari kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifuatilia mafunzo hayo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani kutoka Hospitali ya Rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza, Dkt. Julieth Nkoubi amesema mafunzo hayo ni muhimu na yatawasaidia kufanya tathmini kwa weledi zaidi kwa wafanyakazi wanaoumia kazini.
Daktari kutoka Hospitali ya Magai Kahama, Dkt. Peter Magai akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo ambao ni pamoja na kuwawezesha madaktari kufanya tathmini sahihi kwa wanachama wa WCF wanaoumia kazini.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Madaktari walioshiriki mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala (katikati waliokaa) ambaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza, Amos Makalla (hayuko pichani).
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: