Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akikabidhi tuzo ya OSHA mshindi wa jumla wa maonesho hayo Mkufunzi wa Usalama mahali pa kazi wa Barrick Bulyanhulu, Azaely Kitenge (katikati) ni Mwenyekiti wa Bodi ya OSHA, Dkt. Adelhelm Meru.
Wafanyakazi wa Barrick wakifurahia tuzo mbalimbali ambazo kampuni imenyakua katika maonesho ya OSHA 2023 .
---
Barrick Tanzania imenyakua tuzo sita katika hafla ya utoaji wa tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ya 2023 iliyofanyika mjini Morogoro ambapo Mgodi wa Dhahabu wa Barrick Bulyanhulu, umeshinda tuzo kubwa ya mshindi wa juu wa Jumla katika Tuzo ya Afya na Usalama (OHS) 2023.
Mbali na ushindi huo mkubwa, Bulyanhulu, pia ilinyakua tuzo ya uandaaji Ripoti Bora ya Tathmini ya Hatari katika uchimbaji madini na mshindi Bora wa tuzo ya Usalama na afya (OHS) katika sekta ya madini.
Kwa upande wake, Barrick North Mara, ilishinda tuzo za juu katika: Kujali zaidi Wafanyakazi wenye Mahitaji Maalum na utekelezaji sera bora ya Usalama mahali pa kazi (OHS). Pia ilikuwa mshindi wa pili kwa washindi wa jumla wa sekta ya Madini.
Mwaka huu Mgodi wa Buzwagi pia ulishiriki maonesho hayo na kunyakua tuzo ya utekelezaji Mpango Kazi Bora wa Usalama na Afya mahali pa kazi.
Maonyesho ya OSHA mwaka huu yalifanyika katika viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako, alikuwa mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo za mwaka huu.
Barrick Tanzania imeshinda tuzo za 2023 kutokana na mafanikio ya 2022 ya kampuni ambapo ilishinda tuzo za jumla ikiwemo tuzo ya mshiriki wa maonyesho na tuzo ya kuzingatia kanuni za usalama
Usalama ni sehemu muhimu ya DNA ya Barrick. Kampuni ina mpango maalum kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wake na wakandarasi, kuhakikisha kwamba kila mtu anarudi nyumbani akiwa na afya njema na salama. Juu ya yote hayo katika Barrick kila mtu amejitolea kufanya analoweza kuhakikisha hakuna matukuo ya ajali katika sehemu yake anapofanyia kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: