Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (Mnec) Emmanuel Gungu Silanga kulia akikabidhi cheti maalum kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt Yahaya Ismail Nawanda kushoto, kwa kutambua mchango wake katika maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM.
Na Mwandishi Wetu
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapindizi (CCM) Taifa, Emmanuel Gungu Silanga ametoa Katiba na vitabu vya kanuni, uongozi usalama na maadili za Chama hicho kwa Makatibu Tawi, wa CCM kwa Mkoa mzima wa Simiyu.
Kwa Mujibu wa Mnec huyo lengo la kutoa Katiba na Kanuni ni kuimalisha Chama na Viongozi wake kuelewa masuala mbalimbai yanayotakiwa kufanywa na Chama hicho.
Gungu ametoa vitendea Kazi hivyo muhimu vya Chama, katika maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM ambapo katika Mkoa wa Simiyu yalifanyika kwenye viwanja vya Madeko Wilayani Maswa ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Aidha, Gungu katika kuboresha utendaji wa Chama hicho alisema katika Wilaya ya Meatu Mkoani humo atasaidia ufungwaji wa vipoza joto (Feni) ambapo atatoa vipoza joto hivyo vitano, katika ukumbumbi mkubwa wa CCM uliyopo Wilayani humo, ili Wanaccm wanaotumia ukumbi huo wafanye vikao vya chama katika hali tulivu.
Alisema anamshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kazi kubwa anazowafanyia Watanzania kwa kuleta fedha nyingi na miradi kwa asilimia 90 Jambo ambalo ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
" Mimi kama kiongozi wa chama ninajukumu kubwa la kuhakikisha viongozi wa chama wanajua kanuni na misingi ya chama chetu, hivyo nitatoa kanuni na katiba za chama kwa makatibu wote wa matawu kwa mkoa huu," alisema Gungu nakuongeza:
"Chama chetu nikikubwa kimetimiza miaka 46 Sasa. Najua tumefanya chaguzi na zimemalizika, kilichopo Sasa ni kufanya Kazi ya kuwatumikia Watanzania na Wanaccm wote kwa ujumla, hatuhitaji kuona tena kunakuwa na makundi ndani ya chama."
Kwa upande wa Meatu alisema anajukumu la kuchangia ndani ya chama hivyo ametoa feni Tano katika ukumbi wa chama hicho ili nyakati za joto vikao vifanyike kwa ufanisi.
Maadhimisho ya miaka 46 yalikwenda sambamba na utoaji vyeti vya kutambua mchango wa Watu waliyofanikisha kufanyika kwake, ambapo Mbunge wa Itilima Njalu Silanga na Mkuu wa Wilaya hiyo walitunukiwa vyeti hivyo.
Mapema, Katibu wa CCM Mkoani humo, Mohamed Ally akizungumza katika maadhimisho hayo aliwataka watanzania na wanasimiyu kuacha kuwasikiza Watu wasiokuwa na hoja za msingi.
"Kuna Watu watakuja na hoja ambazo hazina msingi msiwasikilize, CCM ni chama kikubwa na kimefanya mambo mengi nanyie wenyewe mnaona yaliyofanyika,"alisema Ally.
Toa Maoni Yako:
0 comments: