Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati akifungua wa kikao cha wadau cha kujadili na kutathimini mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa miaka minne uliokuwa unaotoa elimu, uwezeshaji na stadi za maisha ( Education Empowerment and Life Skills for Adolescent and Young Children -EELAY) Mkoa wa Tanga tangu Juni 2018 hadi Desemba 2022. kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo.
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo wakati akifungua wa kikao cha wadau cha kujadili na kutathimini mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa miaka minne uliokuwa unaotoa elimu, uwezeshaji na stadi za maisha ( Education Empowerment and Life Skills for Adolescent and Young Children -EELAY) Mkoa wa Tanga tangu Juni 2018 hadi Desemba 2022.
Meneja awa Mradi huo kutoka Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Hope Jassson akizungumza wakati wa kikao hicho
Meneja awa Mradi huo kutoka Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Hope Jassson akizungumza wakati wa kikao hicho
Na Oscar Assenga,TANGA.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa amelishukuru Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania kwa kuwakomboa Mabinti na Wasichana ambao hawakupata elimu kupitia mfumo maalumu,
Mgandilwa aliyasema hayo wakati wa kikao cha wadau cha kujadili na kutathimini mafanikio ya utekelezaji wa mradi wa miaka minne uliokuwa unaotoa elimu, uwezeshaji na stadi za maisha ( Education Empowerment and Life Skills for Adolescent and Young Children -EELAY) Mkoa wa Tanga tangu Juni 2018 hadi Desemba 2022.
Mradi huo ulikuwa na vipengele viwili muhimu,kipengele cha kwanza kinalenga wasichana walioko kwenye rika balehe wenye umri kati ya miaka 15-24 kwa kutoa elimu ya Sekondari ,mafunzo ya stadi za maisha na fursa za ajira kwa wasichana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa kutumia programu ya muda mfupi yenye matokeo chanya kusaidia wasichana katika kukamilisha miaka minne ya elimu ya Sekondari ndani ya miaka miwili.
Alisema kwamba wanashukuru sana kwa mradi huo ambao unawaachia urithi mkubwa wa elimu kwa Watoto hivyo wap kama Serikali wanawaomba wakakae chini watathmini upya kisha warudi tena katika Mkoa huo na Halmashauri ya Jiji la Tanga kuendelea.
Alisema miradi yote ambayo inaachwa na mradi huo itaendelezwa na kwamba hakuna mradi hata mmoja ambao utatelekezwa huku akiwakikishia kuwa miradi yote itaendelezwa kwa gharama yoyote ile na Serikali itasimamia kuhakikisha watoto wanaendelea kupata elimu.
Awali akizungumza Meneja awa Mradi huo kutoka Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Hope Jassson alisema kwamba hadi sasa zaidi ya Wasichana 900 ambao hawakufanikiwa kupata Elimu katika mfumo maalumu wa Elimu ya upili ( Sekondari) wamefanikiwa kupata Elimu hiyo kupitia Mradi wa Elimu na Stadi za Maisha unaotekelezwa katika Mkoa wa Tanga.
Hope alisema Shirika hilo Chini ya Ufadhili wa Shirika la Norad la Nchini wamefanikiwa kuwapatia Elimu ya Sekondari Mabinti hao zaidi ya 900 chini ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,
" Asilimia 86.8 ya Wasichana walioko kwenye Rika Balehe wamefaulu na kupewa Cheti Cha Elimu ya Sekondari kuanzia Mwaka 2017 Hadi 2021, Vituo 30 vya Masomo vinaendelea ya Elimu chini ya usimamizi wa Jamii ambapo Kati ya hivyo Vituo 20 vipo katika Halmashauri ya Jiji la Tanga na 10 vipo Wilaya ya Korogwe " Alisisitiza Hope
Alisema Wasichana zaidi ya 1161 walipatiwa Mafunzo ya kuanzisha Biashara ndogo pamoja na Mitaji kupitia SIDO,VETA na Ustawi wa Jamii,
"Zaidi ya asilimia 65 ya Wasichana hususani katika Halmashauri ya Jiji la Tanga Wanajishughulisha na shughuli za kujiongezea kipato na kubadili mfumo wao wa Maisha ya awali kabla ya kupata Elimu " Alisisitiza Hope
Aliongeza kuwa Wasichana 10 wa wamefanikiwa kujiunga na Chuo kikuu kwa kozi za Shahada ya Kwanza huku Wasichana 22 Walioko kwenye Rika Balehe Wamehitimu ngazi ya Cheti kutoka Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Tanga.
"Wasichana wengine 3 waliandikishwa katika Vyuo mbalimbali vikiwamo chuo Cha maji,chuo Cha Taifa Cha Zanzibar na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha, Watoto 1670 wa miaka 3-5 walipata Elimu ya Makuzi ,Malezi na Maendeleo ya awali, nafasi za kazi zaidi ya 450, Ujenzi wa Madara mapya 22 na Ukarabati wa madarasa 13 pamoja na Walimu 41 wa Elimu ya Awali kutoka Shule za Serikali walipatiwa Mafunzo juu ya Mtaala wa Elimu ya Awali pamoja na kutoa Vifaa vya kufundishia" Alisisitiza Hope.
Toa Maoni Yako:
0 comments: