Na Eleuteri Mangi, WUSM
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaunga mkono juhudi za kuendeleza na kuimarisha shuguli za utamaduni nchini likiwemo Tamasha la Majimaji Serebuka.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amesema hayo Julai 23, 2022 Songea mkoani Ruvuma wakati akifungua Tamasha la Majimaji la Serebuka lililofanyika katika Uwanja wa Majimaji mkoani humo.
“Wizara yetu imefanya jitihada mbalimbali za kukuza, kuendeleza na kulinda utamadauni. Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara imejiweka vipaumbele mahususi ikiwa ni pamoja utekelezaji Mfuko wa Utamaduni na Sanaa wenye lengo la kuwanufaisha wadau wa seka hizi, kuendesha Tamasha la Utamduni la Kitaifa ambalo kwa mara ya kwanza limefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 1 hadi 7 Julai, 2022” amesema Mhe. Gekul.
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa tamasha hilo ambalo ni la wazi kwa kila mtu kushiriki linafanyika Songea mjini lakini ni la Watanzania wote kwa mujibu wa historia yake ambayo ni ya kizalendo kwa taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: