Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza wakati wa kufungua Mafunzo ya waandishi wa habari leo Julai 27,2022 Katika Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango ya Nje, Bw. Justine Kisoka akiwasilisha mada katika semina kwa wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Balozi Mstaafu Peter Kallaghe akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mindi Kasiga akifafanua jambo katika mafunzo ya waandishi wa habari.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara yake na waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali.

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amesema kuwa watahakikisha wanaimarisha mahusiano kati ya wizara na vyombo vya habari nchini ili mabalozi waweze kusikika.

Hayo ameyasema leo Julai 27, 2022 wakati akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika kwa siku mbili katika Chuo Cha Diplomasia jijini Dar Es Salaam. Amesema kuwa mabalozi wamekuwa wakifuatilia mambo mbalimbali nchini.

Amesema kuwa wataendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa sababu ni wadau muhimu kwa manufaa ya nchi yetu.

"Naimani mafunzo haya yatakuwa na faida kubwa kwenu lakini zaidi ni katika kujenga mahusiano ya karibu baina yetu na nyinyi, Wizara na Serikali kwa Ujumla." Amesema Balozi Mulamula

Amesema kuwa waandishi wa habari wanamajukumu ya kuilinda na kuitetea taswira ya Tanzania kupitia kazi wanazozifanya kwa kuzingatia taswira ya nchi wakati wanatekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa Mada Mbalimbali zitatolewa hasa katika kuzingatia masuala ya kidiplomasia ya nchi na nchi nyingine.

“Mhakikishe mnailinda taswira ya nchi, hii ni nchi yetu wote, ikiharibika taswira hata wewe uliyeandika pia utakutana na athari zake, hata uende wapi utajulikana kama Mtanzania." Amesema

Balozi Mulamula amesema mafunzo haya yatakuwa endelevu ili kuwepo na waandishi maalumu watakaokuwa wanaandika masuala ya Kidiplomasia kwa weredi, ikiwemo Itifaki, Diplomasia ya Umma, Uzalendo na Mawasiliano ya kimkakati baina ya Tanzania na nchi zingine.

Pia amewashukuru waandishi wa habari nchini kwa ushirikiano uliopo kati yao na wizara yake na kuwataka kuzingatia mafunzo yatakayotolewa.

Mafunzo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yamewashirikisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya hapa nchini.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula aki na viongozi mbalimbali wakati apowasili Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Jne na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mindi Kasiga wakati alipowasili kwenye Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi Mstaafu Patrick Tsere wakati alipowasili kwenye Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022. katikati ni Balozi Mindi Kasiga Mkurugenzi wa Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula aki na viongozi mbalimbali wakati apowasili Chuo Cha Diplomasia Kurasini Jijini Dar es Salaam kufungua mafunzo ya waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti habari za Diplomasia na ushirikiano wa Kimataifa yanafofanyika kwa siki mbili kuanzia leo Julai 27,2022 na 28, 2022.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: