Na Amiri Kilagalila, Njombe

WANANCHI wa kiijiji cha lgima wilayani Wanging'ombe mkoa wa Njombe wegomea zoezi la anuani za makazi kwa madai ya kutakiwa kuchangia shilingi 80,000 kwa kibao cha kitongoji husika na 4000 kwa kibao cha namba za kila nyumba.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika zahanati ya kijiji hicho wamesema gharama hiyo ni kubwa ukilinganisha na hali ya maisha pamoja na kukosekana kwa elimu juu ya umuhimu wa jambo hilo.

Mmoja wa wananchi Jafari Chaula alisema taarifa ya mwenyekiti yakuchanga vibao kwa 80,000 na 4000 ni kubwa hivyo hawawezi kutengeneza.

"Kwanza nipate elimu kibao cha kwemye nyumba yangu kinafaida gani alafu pili cha kitongoji kinasaidia nini?na nani akichonge?alihoji Chaula,Sisi tumekubaliana hatuchangi kwa sababu hali ngumu,mwenyekiti kawaambie tumegoma"alisema Chaula.

Naye Chesco Mligo alisema changamoto hiyo imewashtua sana wanachi wa kijiji hicho kwa sababu hawajui chochote badala yake wanaambiwa wachonge vibao.

Awali mwenyekiti wa kijiji cha Igima wilayani Wanging'ombe Leonard Ngole,aliwatangazia wananchi kwamba wanatakiwa kuchanga kiasi cha 80,000 kwa kila kitongoji na 4000 kwa vibao vya nyumba.

"Mimi nalirejesha kunapohusika kwa sababu mimi nimeagizwa kuja kuwaelekeza wananchi lakini wananchi wegomea vibao vyote,wao walisema tukusanye fedha tupeleke halmashauri ndipo vibao vije"alisema Ngole.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Lauter Kanoni alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi juu ya swala hilo amesema,wananachi wa kijiji cha Igima waliogomea zoezi la anuani za makazi hawakua na elimu ya kutosha.

"Nimekwenda pale kijiji cha Igima nimeitisha mkutano wa hadhara nikawaelewesha nia na madhumuni wakaelewa changamoto iliyokuwepo wale wananchi walikua wanadhani serikali imetoa hela kwa ajili ya kuwezesha zoezi hilo kwa hiyo nikawaambia hela iliyotoka serikalini ni kwa ajili ya kuwalipa makarani"alisema Kanoni.

Kanoni alisema"Changamoto ya pili ni gharama ya vile vibao kwa maelekezo wayokua wamepewa watendaji kulisimamia zoezi alikua ametafutwa mzabuni mmoja ambaye alikua akiuza kibao kimoja cha namba 4000 sasa shilingi 4000 kuipata kwa mwananchi wa kawaida sasa hivi ni ngumu hivyo tumewaita watendaji kuwapa sampo ya namna gani kibao kitengenezwe wakatafute mafundi wao kwa hiyo tukafikia hapo na mgogoro ukaisha"

Akizungumza kuhusu vibao vya 80,000 mkuu wa wilaya alisema vibao hivyo ni vya kutambulisha mtaa au barabara kiuhalisia gharama zake ndio hizo.

"Mahala pengine wanauza hivyo vibao kwa 100,000 na zaidi lakini alitafutwa mzabuni kutoka wilayani Makete anaviuza hivyo vibao kwa 80,000 mpaka 85,000,tulichokubaliana tutamuelekeza mkurugenzi"alisema Kanoni.

Aliongeza kuwa"Sio lazima kutafuta kwa huyu mzabuni kama wanaweza kukitengeneza kwa gharama nafuu vyenye ubora itakua vizuri"alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: