Nyumba moja mali ya Bw. Rashid Adam mkazi wa Dodoma, imenusurika kushika moto kutokana na gari iliyokuwa imepaki nje ya nyumba hiyo kuteketea kwa moto.
Nyumba hiyo iliyoko jirani na jengo maarufu la "Shoppers Plaza" imenusuruka kushika moto baada ya gari ndogo aina ya Mazda yenye namba za usajili T788 DCJ kuteketea kwa moto likiwa linafanyiwa matengenezo nje ya nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa fundi aliyekuwa anatengeneza gari hilo, chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (M) Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Julishael Mfinanga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusisitiza wananchi kuendelea kuitumia namba ya dharura 114 ili kurahisisha shughuli za kuzima moto na maokozi kufanyika kwa wakati sahihi.
Bw. Rashid Adam (Mmiliki wa nyumba), amelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufika kwa wakati na kuzima moto ambao ungeweza kuleta madhara zaidi kama usingezimwa.
(Picha kwa hisani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Toa Maoni Yako:
0 comments: