Na Amiri Kilagalila, Njombe
Polisi mkoani Njombe imeonya wananchi kujihusisha na vitendo vya ushirikina na kubainisha kuwa yeyote atakayemuita jirani yake mchawi na kukamatwa kwa tuhuma hizo itapelekea kuhukumiwa kwenda jela miaka saba bila ya kuwa na dhamana.
Hayo yamebainishwa na Sajenti Thobias Nyagawa wakati Polisi na idara ya dawati la jinsia na watoto walipofika kijiji cha Itunduma kata ya Mtwango wilayani Njombe kutoa elimu juu ya unyanyasaji wa kijinsi,mauji pamoja na udumavu mambo amabyo yamekuwa yakiwatesa wananchi mkoani humo.
“Kama kuna mtu anatangaza uchawi iwe mwisho,ukimwita mtu mchawi tukagundua,unakwenda jela miaka saba yaani hiyo unakwenda moja kwa moja hakuna dhamana”alisema Sajenti Thobias Nyagawa
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amewaonya vikali vijana wanao subiri kurithi mali za wazazi wao badala ya kufanya kazi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: