Meneja Masoko na Mawasiliano wa Vivo Energy Grace Kijo akizungumza na wanafunzi wa kike wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Kurasini jijini Dar es Salaam, ili kujadili taaluma zao za baadae.
Wafanyakazi wa Vivo Energy
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Vivo Energy Grace Kijo akiwa na Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kurasini jijini Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu
Kampuni ya Vivo Energy, inayosambaza na kuuza mafuta na vilainishi katika kampuni ya Shell na Engen kwa wateja wa rejareja na wafanyabiashara barani Afrika. Leo imetembelea shule ya Msingi na Sekondari Kurasini jijini Dar es Salaam, kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
Wafanyakazi wa Vivo Energy walipata fursa ya kukutana na wanafunzi wa kike wa kidato cha tatu na cha nne katika Shule hiyo ili kujadili taaluma zao za baadae. Walitoa ushauri juu ya njia ya kuchukua, changamoto ambazo wanaweza kukutana nazo. Waliweza kuwapa motisha wasichana wa shule hiyo ya kufanya kazi kwa bidii katika masomo yao na kujua kwamba wanaweza kufikia chochote ambacho wanaweka akilini zao.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Vivo Energy Grace Kijo, alisema “Kama wanawake tunahitaji kujua mwelekeo wa kufuata katika kutafuta taaluma. Uamuzi wako ni muhimu ,unatakiwa kujiamini na utaweza kufanikisha.
Aliendelea kusema kuwa hii ni mara yao ya kwanza kutembelea Shule ya Sekondari Kurasini na wanapanga kurejea ili kusaidia mahitaji mengine ambayo wasichana wa shule hiyo wanaweza kuwa nayo. Hii pia ni sehemu ya mpango wetu wa CSR na tunapanga kuendelea kushirikisha jumuiya yetu.
Vivo Energy pia ilishirikiana na Bora international, shirika lisilo la kiserikali la Dar es Salaam ambalo lilitoa mafunzo kuhusu maandalizi ya kazi. Pia walitoa uzoefu wao na kushauri ni mwelekeo gani wa kupitia.
Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Kurasini Sonia Madaha, “Tuna furaha sana kwamba Vivo Energy wamechagua kutembelea shuleni kwetu. Kama wanafunzi ambao tunamaliza kidato cha 4 hivi karibuni, tunahitaji mwelekeo kuhusu jinsi ya kufikia taaluma tunayotamani. Tunawaalika warudi, kututembelea na pia kutusaidia na mahitaji mengine ambayo sisi wasichana tunahitaji ili tuweze kujifunza kwa usalama.
Toa Maoni Yako:
0 comments: