Asali inayozalishwa na Wakala wa Huduma za Tanzania ( TFS) Wilayani Gairo ikiwa imehifadhiwa.
Sehemu ya mizinga ya kufugua nyuki iliyopo maeneo ya Msingisi inavyoonekana.
Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Gairo Robert Mwangosi ( kushoto) akifafanua jambo kuhusu Ufugaji Nyuki na faida zake.

Na Mwandishi Wetu

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Mhifadhi Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro Robert Mwangosi amesema wamejikita kwenye ufugaji wa nyuki kwa kuwa wana manzuki kubwa sana maeneo ya Msingisi ambayo inafanya vizuri kwenye ufugaji nyuki ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita wamevuna tani moja ya asali kutoka kwenye mizinga 82 tu.

Akielezea zaidi Mwangosi amesema Gairo inafanya vizuri katika suala zima la uzalishaji wa asali ,hata hivyo wamekua wakijikita katika kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuhusu ufugaji wa nyuki.

"Asali ya Fairo inasomeka vizuri katika soko ,imekua na sifa tofauti kwani asali yetu ina sifa ya kuganda kutoka na mimea ya maeneo hayo na mimea tunayoendelea kuipanda kwani tuna mimea inayoitwa Akeshia yale maua yake ndo yanayopelekea asali hiyo kuganda,"amesema.

Pia ubora wa asali ni mzuri na hiyo imefanya asali hiyo hununuliwa na watu wa nje ya Gairo na ndo mana wanaendelea kujikita katika kuwahamasisha wananchi kupanda miti na kuangalia aina ya mimea ambayo inafanya vizuri na inayo pendwa na nyuki na kuweza kufanya vizuri katika uzalishaji wa nyuki.

Kwa upande wake Ofisa Ufugaji Nyuki TFS Gairo Aled Heneriko ameeleza katika msimu huu wa mvua ni msimu wa nyuki kujenga hivyo ameshauri kwa wakati huu mizinga ambayo ilikua ina uchafu isafishwe ili wakati ambao makundi ya nyuki yanapokuwa yanahama kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine yaweze kuingia katika hiyo mizinga kwaajili ya kujipatia mazao mbalimbali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: