Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWASA), Mhandisi Justine Rujomba akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) sehemu ya kuwashia pampu ya kusukuma maji wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya maji safi na uondoaji wa maji taka katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru.
Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWASA), Mhandisi Justine Rujomba akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mchoro wa kituo cha pampu ya kusukumia wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na uondoaji wa maji taka katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo na watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWASA) kabla ya kamati hiyo kwenda kukagua mradi wa kuboresha huduma ya maji safi na uondoaji wa majitaka katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka wakiangalia mitambo ya umeme wakati walipokwenda kukagua mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na uondoaji majitaka katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWASA).
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka wakiangalia kisima cha maji chenye ujazo wa lita milioni kumi walipokwenda kukagua mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na uondoaji majitaka katika Jiji la Arusha na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Arumeru unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWASA). PICHA NA OFISI YA BUNGE
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: