WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Simba leo Februari 13 wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.
Bao la mapema lilijazwa kimiani na Pape Sakho ilikuwa dakika ya 12 kwa pasi ya Shomari Kapombe lilidumu mpaka muda wa mapumziko.
Kipindi cha pili ASEC Mimosas walifanya kweli na kupata bao la kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Aziz Stephan ambaye alitumia vema makosa ya safu ya ulinzi wa Simba chini ya Joash Onyango.
Bao la pili kwa Simba lilipachikwa na Kapombe ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti moja matata ilikuwa dakika ya 78.
Iliwachukua dakika tatu mbele Simba kupachika bao la tatu kupitia kwa Peter Banda ambaye alionyeshwa kadi ya njano kutokana na kuvua jezi wakati anashangilia.
Licha ya ushindi huo ASEC Mimosas walionekana wazuri katika umiliki na waliweza kufanya hivyo kwa asilimia 52 huku Simba ikiwa ni asilimia 48.
Simba inaongoza kundi D ikiwa na pointi tatu kibindoni ina kazi ya kurejeana nao kwa mara nyinginme ugenini Machi 20.
Toa Maoni Yako:
0 comments: