Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akisisitiza jambo kwa viongozi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wakati alipotembelea ofisi za Mamlaka jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt. Agnes Kijazi na Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Hali ya Hew ana Utafiti wa Mamlaka hiyo, Dkt. Ladislaus Chang’a.
Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Agnes Kijazi, kuhusu utendaji wa Mamlaka hiyo wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Hali ya Hewa na Utafiti wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Ladislaus Chang’a, wakati alipotembelea ofisi ya uchakataji taarifa za hali za hali hewa, jijini Dar es Salaam.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini ( TMA) kubuni vyanzo vya Mapato vsivyomkandamiza mwananchi wala kuidumaza Taasisi ili waweze kujiendesha na kuendelea kutoa huduma bora na zenye viwango.
Hayo yamesemwa leo Februari 7, 2022 jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Ally Possi, wakati wa ziara yake ya kikazi TMA kuangalia utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
"Nawapongeza sana ninyi wote lakini kwa kipekee nampongeza Mkurugenzi mkuu, mama yetu mama Kijazi kwa Mapinduzi makubwa sana ambayo umekuwa ukiyafanya kwa sababu Taasisi hii imekuwepo kwa muda mrefu lakini ni kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikifanya Mapinduzi makubwa sana." Amesema Dkt. Possi.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa Taasisi hiyo mpaka sasa imeishapokea sh. Bilioni saba ili ziendelee kuboresha huduma za hali ya hewa na miradi yake mbali mbali.
"Serikali inatoa jicho lake TMA kwa sababu inaona kazi zinazofanywa na Taasisi hii ambazo siyo tu kwa ajili ya nchi yetu pekee bali hata kimataifa na pia zimekuwa zikisaidia ukuaji wa sekta zingine, hususani sekta ya maji na kilimo" amesema Dkt. Kijazi Possi
Ameagiza Taasisi kuhakikisha inafuatiliwa kwa karibu miradi yake ili isichukue muda mrefu kukamilika, iishe kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa ili mwisho wa siku thamani ya pesa zinazotolewa na serikali ziweze kuonekana.
Amesema pamoja na mambo mengine uchumi wa nchi yetu unategemea sana shughuli za bandari na bandari yetu inaweza kuonekana siyo sehemu sahihi sana kwa mizigo kushindwa kufika huku kwetu kama hakutakuwa na Utabiri uliosahihi.
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa ili kuongeza uhakika wa taarifa kwa kuwa sekta ya hali ya hewa inazitegemeza sana sekta nyingine hususani za usafirishaji pamoja na kilimo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, amemuhakikishia Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa Mamlaka imejipanga kikamilifu kuboresha miundombinu pamoja na kusomesha watumishi ili kuendeleza weledi katika sekta hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: