MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akizungumza Bungeni Jijini Dodoma February 11,2022MBUNGE wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira akisisitiza jambo Bungeni Jijini Dodoma February 11, 2022
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu Tanzania Bara kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs)
Mh Neema Lugangira ameiomba Serikali ipitie upya uamuzi wake wa kuiondoa
masuala ya usalama wa chakula kutoka Wizara ya Afya na kuipelekea
kwenye eneo la mambo ya viwanda na biashara badala yake wairudishe
ilipokuwa awali .
Aliyasema
hayo Bungeni Ijumaa tarehe 11 Februari 2022 Jijini Dodoma ambapo
alisema kwa sababu duniani kote masuala ya usalama wa chakula
yanaratibiwa na chini ya wizara ya afya kwa maana chini ya mamlaka ya
kudhibiti ubora wa chakula na dawa na hata kwa Tanzania miaka ya nyuma
tulikuwa tunafanya hivyo chini ya TFDA.
Alisema
hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa Serikali kufanya mapitio na maboresho
ya uamuzi wake kwa kadiri itakavyoona hivyo kwa unyenyevu mkubwa na kwa
maslahi mapana ya kulinda afya za Watanzania ,kulindi mzigo mkubwa
ambao wizara ya afya unaona na mzigo wa ongezeko la magonjwa ya kansa
ambao hauweleki suala la usalama wa chakula lirudi Wizara ya Afya.
Mbunge
Neema alisema hata nchi za Afrika Mashariki zilikuja nchini kuja
kujifunza lakini miaka ya karibuni serikali ilivunja mamlaka hiyo na
badala yake kuunda TMDA na jukumu la usalama wa chakula wakaliweka chini
ya Shirika la viwango (TBS) sasa jambo hilo limeweka maisha na afya za
watanzania herani.
Alisema
anasema hivyo kwa sababu TBS ina jukumu la kuangalia ubora wa
matairi,misumari,mabati na nk na hapo hapo ipewe jukumu la kuratibu na
kudhibiti ubora na usalama wa chakula na hao hao ndio wanatoa kibali kwa
wazalishaji wa chakula .
“Na
hao hao waende kuangalia kile kibali kimekidhi kutakuwa na mgongano wa
maslahi, Mh Naibu Spika kuna jambo mahususi lilijitokeza ambalo ni
dhihiri kwamba TBS haiwezi kuendelea kubeba jukumu la usalama wa chakula
“Alisema
“Kwa
mfano mwaka jana Octoba 2021 Shirika la chakula na madawa la Kenya
lilitangaza kwamba linarudisha juice aina ya Ceres za Apple ambazo
zilikuwa na aina moja ya sumu kuvu ambayo ni hatari kwa maisha ya
binadamu mpaka siku hiyo kwa Tanzania TBS bado ilikuwa haijasema
chochote”Alisema
Mbunge
huyo alisema na gazeti la Mwananchi lilimtafuta Mkurugenzi wa TBS na
anakumbuka alisema mpaka muda wa Octoba 16 mwaka 2021wamejiridhisha
juice hizo zilikiwa hazijaingia nchini na wanaendelea kufuatilia na
wakibaini zimeingia nchini zitazuiliwa .
Alisema
hapo wakauambia umma kila kitu kipo sawa kwa masikitiko makubwa TBS
waliwadanganya watanzania kwa sababu tarehe 22 kwenye kioski kimoja
Jijini Dodoma alikuta juice hizo aina ya Ceres ya Apple yenye Barcode
zile zile zinauzwa na alichukua jukumu la kuipiga picha na kumtumia
waziri mwenye dhamana ya viwanga na biashara na uwekezaji ambaye
alipokea na kusema atalifanyia kazi.
Aliongeza
kwamba baada ya Waziri huyo kupokea alisema ataifanyia kazi hilo
linaonyesha TBS hawakuchukulia kwa umakini jambo la usalama wa chakula
na hawana muda wa kuangalia usalama wa chakula na wanahatarisha maisha
ya watanzania kwa kuendela kulimbikiza mambo mengi ambayo mengine
hayaendani na usalama wa chakula.
Kwa
kuhitimisha Mbunge Neema Lugangira alisema kuwa jambo hili ni mahususi
ambalo limejitokeza na linadhihiridha kwamba TBS haiwezi tena kuendelea
kubeba usalama wa chakula wa watanzania.
Alisema
kwa sababu mwezi Octoba 14 mwaka jana shirika la Chakula na Madawa la
Kenya lilitangaza kwamba linarudisha juice ya Ceres ya Apple ambazo
zilikuwa na aina moja ya sumu kuvu ambayo ilikuwa na hatari kwa maisha
binadamu”Alisema
“Lakini
mpaka siku hiyo TBS ilikuwa haijasema kitu chochote gazeti Mwananchi
lilimtafuta Mkurugenzi wa TBS na nakumbuka alisema mpaka muda wa Octoba
16 mwaka 2021wamejiridhisha juice hizo zilikiwa hazijaingia nchini na
wanaendelea kufuatilia na wakibaini zimeingia nchini zitazuiliwa”Alisema
Mbunge Neema Lugangira.
Alisema
hapo wakauambia umma kila kitu kipo sawa kwa masikitiko makubwa Naibu
Spika TBS waliwadanganya watanzania kwa sababu tarehe 22 kwenye kioski
kimoja Jijini Dodoma alikuta juice hizo aina ya Ceres ya Apple yenye
Barcode zilikuwa zinauzwa na alichukua jukumu la kuipiga picha na
kumtumia waziri mwenye dhamana ya viwanga na biashara na uwekezaji.
Hata
hivyo alisema baada ya Waziri kulipokea alisema kwamba atalifanyia kazi
na kwamba TBS hawachukulia kwa umakini usalama wa masuala ya chakula na
hawana muda wa kuangalia masuala ya usalama na wanaendelea kuhatarisha
maisha ya watanzania kwa kuendelea kulimbikiza mambo mengi ambayo
hayaendani na usalama wa chakula.
"Kwa
unyenyevu Mhe Naibu Spika naiomba Serikali ipitie upya uamuzi wake
kuyaondoa masuala ya Usalama wa Chakula kwa maana ya Food Safety kutoka
Shirika la Viwango TBS ambalo lipo chini ya Wizara inayosimamia masuala
ya Viwanda na Biashara n.k. yaani turudi katika Best Practice na jambo
hili lirudishwe Wizara ya Afya ili kuokoa na kulinda afya na maisha ya
Watanzania, ”Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments: