Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo tarehe 11 Februari 2022 jijini Arusha Tanzania.
Picha ya pamoja meza kuu; Wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mkutano na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Monica Juma akiongoza mkutano huo, kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Peter Mathuki na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Bw. Christophe Bazivamo na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati kutoka Jamhuri ya Kenya Mej. Gen. Dr. Gordon Kihalangwa wakifatilia mkutano.
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (wa pili kutoka kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Tanzania Bara), Mhandisi Felschemi Mramba (wa kwanza kushoto); Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini -Zanzibar, Dkt. Mngereza Miraji (wa pili kulia ) na Kamishna wa Petroli na Gesi Wizara ya Nishati, Bw. Michael Mjinja (wa kwanza kulia )wakifatilia mkutano.
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio na Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila wakifuatilia majadiliano.
Maafisa Waandamizi kutoka Wizara za Nishati Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Mgeta Sabe pamoja na maafisa waandamizi kutoka Taasisi za Nishati wakifuatilia mkutano
Ujumbe kutoka Kenya
Ujumbe kutoka Uganda

Mawaziri wa Sekta ya Nishati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana leo tarehe 11Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa 15 waBaraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya hiyo.

Mkutano huu ulitanguliwa na mikutano ya awali ngazi ya Wataalamu/Maafisa waandamizi uliofanyika tarehe 8 na 9 Februari 2022 na kufuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 10 Februari 2022.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huu umeongozwa na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba (Mb.) ambaye ameambatana na; Katibu Mkuu Wizara ya Nishati – Tanzania Bara, Mhandisi Felschesmi Mramba; Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini -Zanzibar;
Dkt. Mngereza Miraji; Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio; Kamishna wa Petroli na Gesi kutoka
Wizara ya Nishati; Bw. Michael Mjinja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa ujumla.

Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Waziri Makamba aliwakaribisha nchini wajumbe wamkutano huo na kuwahakikishia kuwa mkutano utafanikiwa kuyafikia malengoyake kufuatia uongozi imara wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Peter Mathuki.

Vilevileakaeleza ukanda wa Afrika Mashariki umejaaliwa rasilimali nishati za kutokahivyo, ni wakati sasa kwa kila nchi kuwa na mikakati imara ya kuhakikisha
nishati ya uhakika inapatikana ili kuihakikishia jamii upatikanaji wa huduma
zote zinazohitaji nishati.

“Tukiwatunapitia changamoto za ugonjwa wa COVID-19 tumeshuhudia namna gani nishati zilihitajikakatika kusaidia kuleta nafuu na kuokoa maisha ya wananchi wetu” alisema Mhe.Makamba.

Naye mwenyekiti wa mkutano huo na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt.Monica Juma alitumia nafasi hiyo kuwashukuru Watalamu na Makatibu Wakuu kwa kufanya maandalizi mazuri ya Mkutano huo na kusisitiza kuwa upatikanaji wa umeme wa uhakika ni moja ya viashiria vya kukua kwa uchumi wa nchi yeyote.

Piaakaeleza kukua kwa uchumi husaidia kupunguza utegemeze na hivyo jitihada zamakusudi zinahitajika kuziwesha Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya
uzalishaji wa kutosha viwandani na katika sekta ya kilimo.

Mkutano huu wa 15 wa Baraza la Mawaziri waKisekta la Nishati pamoja na mambo mengine utapitia na kutoa maamuzi juu ya;
Tarifa ya hali ya utekelezaji wa maagizo ya mikutano iliyopita; Hatua iliyofikiwa
hadi sasa katika sekta za Nishati Jadidifu, Nishati ya Umeme na Nishati ya
Mafuta; pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa na Kikanda ya
Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kadhalika mkutano huu utajadili kwa kina
utekelezaji wa mradi wa kituo cha Nishati Jadidifu cha Afrika Mashariki; Mradi
wa Kufua Umeme wa Nsongezi; Mradi wa kufua Umeme wa Murongo/Kigagati (14MW) na Taasisi ya Mamlaka ya udhibiti wa Nishati katika Nchi za Afrika Mashariki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: