Wadau wa Afya wamekutana jijini Dar Es Salaam kufanya tathmini na kuweka mikakati ya kuimarisha matumizi sahihi ya vituo vilivyoanzishwa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Sekta ya Afya kwa njia ya mtandao (Project - ECHO), pamoja na kuendelea kufunga vifaa katika vituo vipya vitakavyofunguliwa hivi karibuni katika Wilaya chache zilizosalia kupata huduma hiyo.

Mpaka sasa tayari vituo 265 vimeshaanzishwa nchi nzima na mikakati inaendelea ya kuongeza vituo zaidi mikoa ya Kusini na Magharibi.Kikao hicho cha wadau kimefadhiliwa na Serikali ya Marekeni kupitia mradi wa CDC unaotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe.Mratibu wa Mradi wa ECHO kitaifa (Project ECHO), Bw. Jacob Lusekelo akiwasilisha ripoti ya tathmini wakati wa kikao cha wadau walipokusanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Dr. Idda Lyatonga, mmoja wa wataalamu wa tathimini na mratibu wa mpango wa mafunzo kwa njia ya Mtandao (Project Echo) akichangia jambo kwenye kikao cha wadau walipokutana Hoteli Sea Scape hivi karibuni.Mtaalamu wa Maabara kutoka TAMISEMI Bw. Alouis Nicas, akichangia jambo kuhusu mafanikio ya mradi huo kwa wataalamu wa afya waliopo Wilayani baada ya vituo kadhaa kufunguliwa na kuanza kutoka huduma.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya Afya walifuatilia kwa karibu kikao cha wadau na wataalamu wa Afya, kujadili namna ya kuimarisha utoaji mafunzo kwa wataalamu kwenye vituo vya afya kwa njia ya mtandao (ECHO)(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: