Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET), mapema leo Januari 25,2022 imewasilisha mada kuhusu uboreshaji wa Mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Kikristo Tanzania (CSSC).
Wasilisho hilo limetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba katika Mkutano huo unafanyika katika ukumbi wa St Gasper Jijini Dodoma ulioanza kuanzia tarehe 24 ambapo utafikia tamati Januari 28 mwaka huu.
Baada ya wasilisho hilo kutoka kwa Dkt. Komba walimu hao walipata nafasi ya kutoa maoni yao juu ya uboreshwaji wa Mitaala hiyo.
Zoezi hilo la ukusanyaji wa maoni linatarajiwa kukamilika Januari 31 mwaka huu ambapo mchakato wa kuboresha Mitaala itachukua muda wa miaka 3 na Mitaala mipya inatarajiwa kuwa darasani mwaka 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments: