Mkuu wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Chang'ombe, Enjinia Joseph Mwanda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2021 wakati wa mahafali ya 51 ya chuo hicho.
Mkurugenzi wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kanda ya Dar es Salaam Angelus Ngonyani akizungumza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2021.
Meza kuu wakiwa katika mahafali ya 51 mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi na huduma daraja la pili na la tatu VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2021.
Baadhi ya wahitimu wa mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Chang'ombe Jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2021.
Na Mwandishi wetu, Globu ya jamii
JAMII imetakiwa kuondokana na mtazamo hasi kuwa wanafunzi wanaoenda kusoma kwenye vyuo vya kati vya ufundi ni wale waliofeli na kushindwa kuendelea na masomo.
Ameyasema hayo Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)- Dar es Salaam, Injinia Joseph Mwanda wakati akizungumza kwenye mahafali ya 51 ya Chuo cha VETA jijini Dar es Salaam leo Desemba 13, 2021.
Amesema wapo watu ambao wamekuwa wakiyapuuza masomo ya ufundi kutokana na dhana kuwa ni walioshindwa masomo, mtazamo huo umekuwa ukipelekea vijana wenye vipaji kushindwa kuendeleza uwezo wao mbalimbali wa kibunifu ambao ungeweza kuwa na tija kwa taifa.
Amesema kuwa mafunzo ya ufunzi duniani kote ni mafunzo muhimu kwa kuwa wahitimu wa kozi za ufundi ni watendaji wazuri kwenye sehemu hasa za uzalishaji na wanatagemewa.
Amebainisha kuwa kama jamii ikitambua nafasi ya mafundi na kuwalipia ada watoto wao kusomea ufundi wa aina mbalimbali itasaidia kupunguza tatizo la ajira.
Alisema kuwa wahitimu kutoka VETA wamekuwa wakiajiliwa katika viwanda mbalimbali huki wengine wakishika wadhifa wa kuongoza vitengo.
”Kwa sasa kuna wimbo wa Tanzania ya viwandam, sasa huu ni wimbo ambao hakika unataka uwepo wa wataalamu wengi kwenye viwanda na wenye ujuzi mbalimbali." Amesema
Kwa kutambua hilo VETA imeshajipanga kwa kutoa mafunzo bora kwa wanafunzi yatakayowawezesha kupeleka ujuzi wao kwenye viwanda hivyo, sasa ni muda kwa wazazi kuchangamkia kuwaleta vijana wao VETA ili nchi iwe na wataalamu wengi na siyo kwamba VETA ni chuo cha waliofeli.”
Amesema kuwa pia kumekuwa na changamoto ya idadi ndogo ya wanawake kusomea masomo ya ufundi ambapo amebainisha kuwa wanawake wengi wamekuwa na dhana ya kuwa masomo hayo ni ya wanaume tu.
Injinia Mwanda amesema wapo wanawake ambao wamekuwa wakifanya vema kwenye masomo mbalimbali chuoni hapo na kuwa chuo kimeweka mfumo mzuri wa kuwawezesha wanawake kusoma kwa ufanisi.
Amesema ”Wanawake masomo ya ufundi pia yanawafaa tena sana kwa kuwa wanaweza kufanya karibia kila kazi ya ufundi na wapo ambao wamehitimu hapa na wamekuwa wafanyakazi wakubwa na wazuri tu huko walipo.”
Wanafunzi 641 wamehitimu masomo yao katika fani mbalimbali ambapo walipata wasaha wa kuonesha uwezo wao wa mafunzo kivitendo kwa wageni waliofika chuoni hapo.
Kwa upande wake Mkuu wa Section wa Fani ys Uchapishaji, Bernald Nyirenda amesema kuwa wanafunzi waliosoma fani ya uchapishaji wanaajilika kwani wamefunzwa vizuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments: