Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akitazama dawa zilizotengenezwa kwa ajili ya kujikinga na mbu katika maonyesho yaliyofanyika wakati wa Uzinduzi Mpango wa Kukabiliana an Ugonjwa wa Malaria kwa Nchi za Maziwa Makuu za Afrika Mashariki, aliye upande wa kulia kwake ni Waziri wa Afya wa Rwanda Dkt. David Ngamije.
Mtaalamu wa kupambana na mazalia ya mbu akiweka viuatifilu katika ndege isiyo na rubani kwa ajili ya upuliziaji wa dawa hiyo ya kuwa mazalia ya mbu, shughuli hii imefanyika wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Kukabiliana an Ugonjwa wa Malaria kwa Nchi za Maziwa Makuu za Afrika Mashariki ambapo kwa Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Afya
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel (katikati) akiteta jambo na Waziri wa Afya nchini Rwanda Dkt. David Ngamije (kulia) wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Kukabiliana an Ugonjwa wa Malaria kwa Nchi za Maziwa Makuu za Afrika Mashariki uliofanyika katika Wilaya ya Kirehe Nchini Rwanda. Aliye upande wa Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbunge.
Ndege isiyo na rubani (drone) ikiwa angani tayari kwa ajili ya upuliziaji viuwatilifu katika shamba la mpunga eneo ambalo kuna mazalia ya mbu. Hii ni afua mojawapo ya kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mtaalam akipulizia dawa ndani ya nyumba katika kuta, hii ni afua mojawapo katika Mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa Malaria uliozinduliwa katika wa Mpango wa Kukabiliana an Ugonjwa wa Malaria kwa Nchi za Maziwa Makuu za Afrika Mashariki.
Viongizi kutoka Rwanda, Tanzania, Kenya, Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, wakitazama ndege isiyo na rubani (drone) ambayo itatumika kwa ajili kupulizia dawa viuwatilifu kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria kwa Nchi za Maziwa Makuu za Afrika Mashariki ambapo kwa Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: