Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akizungumza wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), kwenye kilele cha Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Novemba 14, 2021. Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama Bw. James Mdlowe alimueleza Mhe. Katambi kuwa katika kipindi cha Wiki moja, karibu watu 300 walitembelea kwenye banda la Mfuko huo ambao umeanzishwa kiasi cha miaka mitatu iliyopita kufuatia uamuzi wa Serikali wa kuunganisha Mifuko. "Katika Wiki hii tulikuwa pamoja na wenzetu wa NSSF hivyo ilikuwa rahisi kwa wanachama wetu endapo wanahitaji ufafanuzi kutoka Mifuko yote miwili basi inakuwa rahisi kutufikia bila ya kuwa na usumbufu wowote kwa wanachama. Kwa upande wake Mhe. Katambi aliwapongeza wafanyakazi hao wa PSSSF kwa kazi nzuri waliyoifanya kwenye Wiki hiyo. " Aliiponhgeza PSSSF kwa kuingia kwenye Mfumo wa Kimtandao ambao mwanachama anaweza kupata taarifa sahihi za Mfuko kupitia simu yake ya kiganjani." Alisema Mhe. Katambi. Wengine pichani kutoka kushoto kwenda kulia ni Bi. Winfrida Jorry, Afisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja, Bw. James Mlowe, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. Abdallah Juma Afisa Mafao Mwandamizi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Bw. Deogratius Marwa, Afisa Matekelezo Mwandamizi.
Mhe. Katambi akiweka saini kwenye kitabu cha wageni.
Mhe. Katambi akiweka saini kwenye kitabu cha wageni, huku Bi. Winfrida Jorry, Afisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja, akishuhudia
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akizungumza wakati alipotembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). Katikati ni Bw. James Mlowe, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama na kushoto ni Bi. Winfrida Jorry, Afisa Mwandamizi Huduma kwa Wateja.
Bw. Abdallah Juma Afisa Mafao Mwandamizi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) akimuonyesha mwanachama hali ya michango yake kutoka kwa mwajiri
Wateja wakiwa kwenye banda la PSSSF, wakihudumiwa
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: