Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo ameshauri uongozi wa halmashauri nchini kuhamasisha vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM na vijana wengine wazalendo kujitoa na kushiriki ujenzi wa miundombinu na miradi mingine ya maendeleo inayoendelea katika Halmashauri hizo.

Ndg. Chongolo ameseme vijana hao wanaweza kusaidia Halmashauri hizo kwa kujitoa na kushiriki kufyatua tofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ambao unaendelea nchi nzima na miradi mingine ya maendeleo.

Katibu Mkuu ametoa ushauri huo tarehe 18 Novemba, 2021 alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Nyumba tano za watumishi katika hospitali ya wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.

“Tunaweza kutumia vijana wa UVCCM wakajitolea kufyatua tofali na tunakuwa na benki ya tofali Kwa ajili ya Ujenzi wa miradi kama hii (Hospital ya Wilaya Kasulu), tunawahamasisha wanakuja, mnanunua unga, maharage siku nyingine mbuzi inachinjwa, tofali zinafyatuliwa na kuchomwa na mnakuwa na benki ya tofali za Ujenzi," amesema.

Katibu Mkuu amefanunua kuwa, vijana wakifyatua na kusaidia kwenye kazi za Ujenzi kama madarasa Halmashauri hizo zinaweza kuwapa heshima ya kutambua juhudi zao Kwa kuweka kumbukumbu ambyo inatambua kuwa mradi husika umejengwa na Halmashuri Kwa mchango wa Vijana wa UVCCM, pamoja na kuwapa kazi nyingine kwa malipo.

Ndg. Chongolo alitoa mfano wa shule Sayansi ya Sekondari ya Dr Joyce Ndalichako iliyopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera ambapo vijana wa UVCCM walijitoa na kufyatua tofali zaidi ya elfu 35 na kuweka benki ya tofali katika shule hiyo na yalitumika kujenga madarasa na maabara ya shule hiyo.

Ameeleza kuwa, hatua hiyo itaongeza kasi ya Ujenzi kuleta thamani ya pesa katika utekelezaji wa miradi husika.

Amesema kutumika Kwa vijana kujitoa kufyatua yofali utaondoa gharama kama vile za kukodi watu kufyatua au kununua tofali, na kazi nyingine ambazo vijana hao wanaweza kuhamasishwa kufanya na kupunguza gharama za kuwalipa wataalamu wengi kusimamia mradi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: