Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Naibu Meya wake Calvas Joseph akiwfuatiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mkoba |
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Spora Liana akizungumza wakati wa kikao hicho |
DIWANI wa Kata ya Chumbageni Ernest Kimaya akiuliza swali wakati wa kikao hicho |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
Mkuu
wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha biashara ya madanguro maarufu kama madada poa inakoma mara moja Jijini humo
DC Mganndilwa alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha cha baraza la madiwani wa halamashauri ya jiji la Tanga ambapo aliyataja maeneo hayo kuwa ni Sabasaba na barabara ya Uhuru na
kusema kuwa wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji
mingine.
"Kuna maeneo
kwetu sisi bado kuna, madanguro ambayo dada zetu wanajiuza naomba
nitumie hadhara hii kwakuwa vyombo vya dola vipo hapa niwaombe tuanze
kushughulika na hawa watu natamani tuone mji wetu unakuwa safi hatutaki
kuona hizi biashara za kujiuza jeshi la polisi wakati nikifanya
opereshen zenu basi mshughulike na watu hawa, "alisistiza DC Mgandilwa.
Katika
hatua nyingine Mgandilwa amesema pamoja na hayo analipongeza jiji hilo
kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutaka kuwalipa fidia
wananchi ambao bado wana migogoro ya fidia zao lengo ni kuondokana na
migogoro isiyokuwa na lazima.
Kwa
upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amewataka
wakuu wa idara kuheshimu maamuzi yanayofanywa na baraza la madiwani ili
kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima inayoweza kukwamisha
jitihada za maendeleo kwenye jiji hilo.
"Nitoe
angalizo kwa wakuu wetu wa idara na watumishi wote wa halmashauri
wapatao 3000 waelewe kwamba kikao cha mwisho chenye maamuzi katika jiji
hili ni baraza la madiwani hivyo wasijaribu wala wasiwaze kujikweza
kimadaraka hakikisheni sheria kanuni taratibu na miongozo zinafuatwa ili
tusifikie kwenye migongano, "alisistiza Meya Shiloo.
Mkurugenzi
wa jiji la Tanga Spora Liana amesema Halmashauri hiyo itatoa taarifa ya
kila matumizi ya fedha yanayofanywa kwa wananchi lengo ni kuweka wazi
kwa kila mwananchi kufahamu fedha za maendeleo zinazotolewa kwenye
maeneo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: