Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi (kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Singida akifungua kikao hicho kilichofanyika jana mkoani hapa. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba na Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt. Angelina Katambi.
Makamu Mwenyekiti wa kikao hicho. ambaye ni Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, akizungumzia mafanikio makubwa yaliyofanywa na Tanroads na Tarura ya kutengeneza barabara katika mkoa huo.
Baadhi ya wabunge wakiwa katika kikao hicho,. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Masare, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau na Mbunge wa Singida mjini, Musa Sima.
Mratibu wa Mkoa wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini Nchini (TARURA) Mhandisi Boniface Magani, akielezea utekelezaji wa mipango ya matengenezo ya barabara hadi kufikia Deseba 30, 2020.
Mbunge wa Manyoni Mashariki, Dkt. Pius Chaya akichangia jambo kwenye kikao hicho kwa kuwapongeza Tanroad na Tarura kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutengeneza barabara na kufika kwa wakati eneo lenye changamoto baada ya kupewa taarifa.
Mwenyekiti wa wabunge wote wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akizungumzia kazi kubwa iliyofanywa na Tanroad na Tarura ya kutengeneza barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.
Mbunge wa Singida Mjini, Musa Sima akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, James Mkwega akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, Hussen Simba, akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Abubakar Muna, alichangia jambo kwenye kikao hicho kwa niaba ya mbunge huyo.
Washiriki kutoka wilaya zote za Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao hicho. Kushoto ni Kaimu Afisa maendeleo Vijana Mkoa wa Singida, Frederick Ndahani.
Wabunge wakiwa kwenye kikao hicho.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Wakuu wa Wilaya wakishiriki kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni, Jumanne Mlagaza, akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida , Eliya Digha, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ali Mwanga, akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Godwin Myovela na Doto Mwaibale, Singida.
WAJUMBE wa Bodi ya Barabara mkoani hapa wamepongeza kasi ya matengenezo ya barabara zilizo chini ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na kuwataka kutobweteka, badala yake waharakishe kukamilisha barabara na madaraja muhimu kwa ukuaji wa uchumi, ili kupunguza kero na kuchagiza maendeleo mkoani hapa.
Wakichangia kwa nyakati tofauti kwenye kikao hicho jana, pamoja na kupongeza kazi kubwa inayofanywa na wakala hizo, waliwataka kuongeza usimamizi wa karibu kwa wazabuni ili kuongeza ufanisi.
Pia ufinyu wa bajeti katika utekelezaji wa miradi mipya na ile ya umaliziaji ikiwemo barabara na madaraja bado ni changamoto jambo linalopelekea kupunguza ari na ustawi wa kiuchumi kwa wanasingida.
Aidha, wamependekeza miradi inayojengwa na wakala hizo iende sambamba na uwekaji wa taa za barabarani ili kuwawezesha wajasiriamali kufanya biashara zao hadi usiku.
Sambamba na hilo, wajumbe hao wameomba kuwapo kwa ukaguzi na matengenezo ya kawaida ya barabara mara kwa mara ili kuongeza tija na uimara badala ya kusubiri wakati wa majanga.
"Nawapongeza sana wenzetu hawa wa Tanroads na Tarula pamoja na fedha ndogo wanazopata lakini wanajitahidi sana...naamini wakipata fedha za kutosha watafanya makubwa kuliko haya," alisema Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu.
Akiwasilisha utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara kuanzia Julai hadi Desemba 2020, Meneja wa Tanroads Mkoa wa Singida, Mhandisi Matari Masige alisema mpaka sasa sehemu kubwa ya mtandao mkoani hapa inapitika.
"Kwa ujumla asilimia 62.7 ya barabara zote zipo katika hali nzuri, asilimia 27.9 zina hali ya wastani na asilimia 9.4 zina hali mbaya," alisema.
Masige alisema kutokana mvua kubwa zilizonyesha mwaka jana na baadhi ya barabara kupandishwa daraja kutoka wilaya kuwa za mkoa imepelekea baadhi kuwa katika hali mbaya na juhudi za matengenezo zinaendelea.
Alizitaja barabara hizo kuwa ni Iyumbu Magereza yenye kilometa 123.7, Sepuka Mgungira kilometa kilometa 89.6 na Soweto Kisiriri Chemchem kilometa 43.3.
Hata hivyo Masige alisema matengenezo ya kawaida kwa barabara kuu hadi mwezi Desemba 2020 yametekelezwa kwa asilimia 53 kikazi na asilimia 2.1 kifedha.
"Kwa upande wa barabara za mkoa kwa matengenezo ya kawaida utekelezaji wake umefikia asilimia 77.7 kikazi na asilimia 45.3 kifedha," alisema Mhandisi Masige.
Tanroads Mkoa wa Singida unahudumia jumla ya kilometa 1,727.6 za barabara Kuu na zile za Mkoa. Kati ya hizo, kilometa 484.2 ni lami sawa na asilimia 28 na sehemu iliyobaki yenye urefu wa km. 1,243.4 sawa na asilimia 72 ni changarawe.
Kwa upande wake, Mratibu wa Tarura mkoani hapa, Mhandisi Boniface Magani alisema hali ya barabara zake mkoani hapa nayo imeendelea kuimarika.
"Kwa sasa hali ya barabara inaridhisha ambapo asilimia 43.21 ya barabara hizo sehemu kubwa inapitika baada ya kufanyiwa matengenezo," alisema.
Magani alisema Tarura Mkoa wa Singida una mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 5,669.412 ambazo zimeingia katika mfumo wa 'Droma.' (Neno la Kigiriki likimanisha miundombinu ya barabara).
Alisema kati ya hizo barabara za wilaya zina jumla ya kilometa 1946.082, barabara za mjazio kilometa 2860.147 na zile za wananchi ni kilometa 863.183.
Toa Maoni Yako:
0 comments: