Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Chama cha Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Meneja wa Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Singida, Agness Yesaya akionesha katiba ya chama hicho baada ya kukizindua chama hicho kwenye hafla iliyofanyika jana mkoani hapa. Kushoto kwake ni Meneja wa TIA, Kampasi ya Singida, Dkt. Jmes Mrema.
Meneja wa Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Singida, Agness Yesaya, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Meneja wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Dkt.James Mrema, akitoa taarifa wakati akimkaribisha Meneja wa Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Singida, Agness Yesaya (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Chama cha Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) wa Taasisi hiyo iliyofanyika jana mkoani hapa. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Chuo cha Utumishi Mkoa wa Singida, Lameck Sospeter na Mwenyekiti wa EWURA Mkoa wa Singida, Bertha Mlingi.
Mlezi wa Chama cha Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida, Jackson Payowela, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Janeneema Makulu akizungumza.
Viongozi wa chama hicho wakimsubiri kumpokea mgeni rasmi.
Mratibu wa Taaluma TIA, Kampasi ya Singida, Shisalalyandumi Ulomi, akizungumza.
Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa chama chao.
Hafla ikiendelea.
Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa chama chao.
Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa chama chao.
Hafla ikiendelea.
Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Charity Mbiriti, akisoma hotuba ya wanafunzi mbele ya mgeni rasmi..
Wanafunzi wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa chama chao.
Wanafunzi wakiserebuka baada ya kuzindua chama chao.
Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala TIA, Kampasi ya Singida, Mtogo Kagulu, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Rais wa Serikali ya Wanachuo, TIA, Kampasi ya Singida, Dauda Dauda, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Na Dotto Mwaibale, Singida
WANAFUNZI wa fani ya Usimamizi wa Rasilimali Watu (HRMA) Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida wameunda chama chao lengo likiwa ni kuwakutanisha na kuwaweka pamoja.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa chama hicho Meneja wa Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Singida, Agness Yesaya akizungumza juzi na wanafunzi hao aliwapongeza kwa kuanzisha chama hicho na kueleza kuwa wanafunzi wa fani hiyo ni watu muhimu sana katika muktadha mzima wa kusimamia na kulinda rasilimali za nchi yetu.
"Ninyi ni watu muhimu sana hapa nchini hasa katika soko la kiuchumi tunawakaribisha Sido mje tuwafundishe mbinu za kutengeneza mashine na bidhaa mbalimbali tutawapa ushirikiano" alisema Yesaya.
Yesaya aliwaambia wanafunzi hao kuwa baadhi yao wataajiriwa serikalini na sekta binafsi lakini ni muhimu pia kupata mafunzo ya ujasiriamali yanayotolewa na Sido ili waweze kujiajiri badala ya kutegemea kuajiiriwa tukizingatia kuwa hivi sasa kuna changamoto ya ajira.
Meneja wa TIA Kampasi ya Singida Dkt.James Mrema akitoa taarifa ya chuo hicho wakati akimkaribisha mgeni rasmi alisema Kampasi hiyo ya Singida ni miongoni mwa kampasi sita za Taasisi ya Uhasibu Tanzania ambayo makao makuu yake yapo Kurasini jijini Dar es Salaam.
Alitaja kampasi zingine kuwa ni Mbeya, Mwanza, Mtwara, Kigoma na makao makuu Dar es Salaam na kuwa kampasi ya Singida ilianzishwa mnamo mwaka 1974 ikiwa na programu mbili za Uhasibu na Masoko.
Dkt.Mrema alisema tangu kampasi hiyo ilipoanzishwa kumekuwepo na ongezeko la udahili wa wanachuo na kuwa sasa kina idadi ya wanachuo 2,242 kati yao wavulana ni 1,099 sawa na asilimia 49 na wasichana wakiwa ni 1,143 sawa na asilimia 51.
Meneja huyo wa kampasi hiyo alisema hivi sasa idadi ya programu zimeongezeka hadi kufikia nne ambazo ni Uhasibu, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Biashara, na Uongozi wa Rasilimali Watu ambazo zote zinatolewa kuanzia ngazi ya astashahada, stashahada na shahada.
" Pamoja na mafanikio hayo kampasi yetu bado inakabiliwa na changamoto kama vile uhaba wa madrasa, mabweni, mwitikio mdogo wa wakazi wa Mkoa wa Singida kuchangamkia fursa ya elimu na kujiunga na chuo chetu kwani asilimia kubwa ya wanachuo wanatoka mikoa mingine.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa chama cha wanafunzi wa fani hiyo ya Usimamizi wa Rasilimali Watu Kampasi ya Singida, Charity Mbiriti alisema chama hicho kiliundwa April 12, 2016 ambapo kilianzishwa katika Kampasi ya Dar es Salaam na sasa kimekusudia kuunganisha kampasi zote ili kuwaweka pamoja.
Mbiriti alitaja malengo ya chama hicho mbali ya kuwaunganisha pia ni kupata warsha na mafunzo ya fani hiyo na yote yanayohusu jamii kwa ujumla, kuhakikisha wanafunzi wanapata uelewa juu ya usimamizi wa rasilimali watu na umuhimu wake katika jamii kwa ujumla, kutengeneza mtandao wa kimasomo kati ya vyuo mbalimbali ili kuleta tija katika fani yao.
Aidha Mbiriti alitaja malengo mengine ya chama hicho kuwa ni kuleta fursa kwa wanafunzi kujitengenezea uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa pamoja na kuimarisha mahusiano mazuri na vyama vingine vya taaluma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: