MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School ya Jijini Tanga Andrew Gasper akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya Coastal Sec City Cup ambayo yalianza kutimua vumbi Machi 5 mwaka huu kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu Yonas Mshigati na kulia ni Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Coastal Sekondari Salimu Mwakimuna.
Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Coastal Sekondari Salimu Mwakimuna aksisitiza jambo wakati mkutano wao na waandishi wa habari kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu Yonas Mshigati
Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu Yonas Mshigati akizungumzia mashindano hayo kulia ni Mwakilishi wa Kiwanda Mamujee Limited ambao ni wadhamni Kiwanda ,Steven Malupa
Mwakilishi wa Kiwanda Mamujee Limited ambao ni wadhamni Kiwanda ,Steven Malupa akielezea jambo kwenye mkutano huo
NA MWANDISHI WETU, TANGA.
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School ya Jijini Tanga Andrew Gasper amesema mbinu kubwa ambayo itasaidia kuiwezesha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kufanya vizuri kimataifa ni wadau na serikali kujikita kuweka nguvu ya pamoja kuandaa wachezaji wazawa kuanzia ngazi za chini kupitia Mashindano ya Umitashumta,Umiseta na Vyuo Vikuu.
Mwalimu Andrew aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mashindano ya Coastal Sec City Cup ambayo yalianza kutimua vumbi Machi 5 mwaka huu kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Galanosi Jijini Tanga.
Shule ambazo zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo ambayo yanatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa ni Coastal Sekondari,Galanosi Sekondari,Chumbageni Sekondari,Old Tanga Sekondari,Usagara Sekondari,TangaTechSekondari,Mkwakwani Sekondari,Japani Sekondari, Masechu Sekondari na Nguvumali Sekondari.
Alisema Mashindano hayo yatakuwa chachu ya kuhakikisha wanapatikana wachezaji wa ndani walio bora zaidi kwa ajili ya timu ya Taifa wana vijana wa chini ya miaka U- 20,U- 17,na Taifa limekuwa likifanya vibaya kutokana na wachezaji wa ndani kukosa misingi imara.
Alisema kwamba iwapo wachezaji ambao wanatoka kwenye mashindano hayo wataendelezwa wanaweza kuja kuwa hazina kubwa kwa Taifa na hivyo kuipeleka nchi kwenye mashindano makubwa Duniani na kuweza kunyakua makombe mbalimbali
“Tukiweka nguvu kwenye ngazi za shuleni nadhani tunaweza kupata timu ya Taifa imara ambayo inaweza kushinda timu yoyote duniani..msingi wa Uganda kama nchi wameweza kufanya vizuri na hiyo imetokana na uwekezaji ambao wameufanya kuanzia ngazi za chini”Alisema Mwalimu huyo.
Mwalimu huyo alisema kwamba kama wataweza kujikita kwenye mashindano ya ngazi ya Sekondari na Msingi wanaweza kufika mbali kimataifa kama Taifa huku akisisitiza kwamva sera ya nchi kwenye michezo lazima iweze kutekelezwa kwa vitendo ili iweze kuwa na tija.
“Mimi nadhani sera ya nchi hata kwenye michezo lazima iweze kutekeleza kwa vitendo na sio maneno na wawepo walimu ambao wanasimamia michezo na hii itakuwa ni chachu kubwa kwa vijana ambao wanaweza kutumia vipaji vyao vya soka kuweza kupata mafanikio”Alisema
Alisema iwapo wachezaji wanaoshiriki kwenye michezo mbalimbali mashuleni watafuatiliwa na kupewa nafasi itasaidia kupunguza tabia ya vilabu vikubwa kama Simba na Yanga kuchukua wachezaji wengi wa kimataifa na kuwaache ya ndani.
Mwalimu huyo alisema misngi ya michezo kama Taifa ilikuwa imebomolewa na kutokutuliwa mkazo zamani miaka 90 wakati wa Rais Mwinyi michezo ya Umiseta ilikuwa na nguvu kubwa na ilikuwa ikizalisha wachezaji wengi sana wa ndani ambao walikuwa na ubora wa kushindana ndani na nje.
Alisema lakini wakati alipoingia Madarakani Rais Mstaafu Marehemu Benjamini Mkapa michezo mashuleni ilianza kudidimia na wakati wa Jakaya ikashika kasi na hata wakati wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli michezo imeendelea kupaa juu zaidi na kurudi kwenye wakati wake.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu Yonas Mshigati alisema kwamba lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji kwenye shule za Sekondari huku akieleza michezo itakayochezwa kuwa ni mchezo wa mpira wa miguu na pete na wanawakaribisha wadau mbalimbali ikiwemo wadhamini.
“Nitoe wito kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kujitokeza kuangalia vipaji mbalimbali kwenye mashindano hayo ambavyo vinaweza kuwa chachu kwenye timu ya Taifa za vijana na baadae kuwa hadhina kubwa ya Taifa”Alisema
Hata hivyo Mwakilishi wa Kiwanda Mamujee Limited ambao ni wadhamni Kiwanda ,Steven Malupa allisema wao wamekwenda kudhamini mchezo wa mpira wa miguu na pete kwa ajili ya kusapoti michezo ili kukuza vipavi kuanzia ngazi ya chini lengo likiwa kukuza soka hapa nchini.
Kwa upande wake Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Coastal Sekondari Salimu Mwakimuna alisema wapo kwa ajili ya kuendesha mashindanbo hayo akiwa kama mwakilishi kutoka shule ameisa jamii na wakuu wa shule za sekondari watoe kipaumbele kwa michezo.
Alisema kwa sababu wanafunzi wanaposhiriki kwenye michezo taaluma yao inapanda ikiwemo kupunguza utori wa reja reja kwa wanafunzi hatua inayowafanya kujikuta wakipenda kuhudhuria shuleni
“Lakini hata matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka jana kwa shule ya Coastal High School tulifanya vizuri vizuri kwa kushirika nafasi ya kwanza Tanga Jiji na kimkoa nafasi ya tatu na nafasi ya 38 kitaifa na yamechagizwa na michezo ..nimpongeza mkuu wa shulke ya Sekondari Coastal Andrew Gaspar kwa kuja na wazo hilo la kuanzisha michezo”Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments: