Kijiji cha Jamii kilichopo katika uwanja wa shule ya msingi Mandela kata ya Pasua ambacho kimendaliwa na Baraza la Watu wanaoshi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) kwa ajili ya kuendesha mijadala juu ya masuala ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
Mwenyekiti wa Baraza la Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Leticia Maurice akizungumza wakati wa mjadala katika kijiji cha Jamii kilichowakutanisha viongozi wa dini mbalimbali nchini.
Baadhi ya washiriki wa mjadla juu ya masuala mbalimbali ya Ukimwi wakifuatilia kwa karibu hoja zilizokuwa zikitolewa katika kijiji cha jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt Leonard Maboko akizungumza wakati wa mjadala katika kijiji cha jamii uliowashirikisha viongozi wa dini .
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la taifa la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Deogratius Rutatwa akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Askofu wa kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la Bonde la Ufa, Marco Barnabas akizungumza katika kongamano hilo .
Katibu wa Baraza la Ulamaa taifa ,Sheakh Hassan Chizenga akizungumza katika kongamano hilo.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo wakichangia mjadala pamoja na kuuliza maswali kwa viongozi wa dini katika kongamano hilo.

Na Dixon Busagaga - Kilimanjaro

BARAZA la Taifa la Watu wanaosihi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) limepongeza hatua ya serikali kuendelea kutoa bure Dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na ugonjwa huo ,dawa zinazotajwa kuongeza seli za kupambana na maambukizi (CD4) kwa haraka ukilinganisha na dawa zilizokuwa zikitolewa hapo awali.

Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (NACOPHA) Leticia Mourice wakati wa kongamano lililoshirikisha viongozi wa dini mbalimbali katika kijiji cha jamii kilichopo uwanja wa Mandela mjini Moshi ambao maadhimisho ya siku ya Ukiwmi Duniani yanafanyika kitaifa.

“Nina ishukuru Serikali kwa kuendelea kutupatia dawa bure ambazo kwa kweli dawa hizo ni nzuri sana ,ni tofauti na zile ambazo tulikuwa tuna meza siku za nyuma ,zinapandisha CD4 haraka ,zinaboresha afya haraka ,yaani pongezi nyingi sana kwa serikali “ alisema Leticia.

Alisema uwepo wa kijiji cha jamii katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani kumechangia wengi wa washiriki kufahamu mambo mengi kuhusu Ukimwi kutokana na mijadala katika kijiji hicho ambapo pia washiriki walipata nafasi ya kuuliza maswali .

“Naamini kabisa kila mmoja wetu amevuna chochote ,tumekuwa na viongozi wa dini kwenye mjadala na wamewaeleza vijana na watu wazima kwamba miili yetu ni hekalu na hili hekalu linapaswa kuwa safi na tunapaswa kuitunza miili yetu .”alisema Leticia .

“Sambamba na hilo tumepata maelezo mazuri kabisa kutoka kwa viongozi wetu wa dini ,sasa kutokana na majadiliano haya mnatakiwa kuwa mashujaa wa kusema hapana ,sihitaji,sipendi kwa habari ya ngono isiyo salama na msiende kuwa mashujaa wa kuwa na watu wengi wa kucheza nao shoo.”aliongeza Leticia.

Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt Leonard Maboko akatumia jukwaa hilo kuwaeleza viongozi wa dini kuwa mlango uko wazi kwa tume anayoingoza endapo kuna masuala mbalimbali ambayo wanegpenda kuyafahamu zaidi.

Kongamano hilo ni muendeleze wa mambo kadhaa yanayofanyika ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo kitaifa yanafanyika mjini Moshi katika uwanja wa shule ya msingi Mandela uliopo kata ya Pasua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: