MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Jiji la Tanga
Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo

Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uchaguzi huo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza na waheshimiwa madiwani kabla ya kuanza uchaguzi huo

Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akiwa na Mstahiki Meya mpya wa Jijini la Tanga (CCM) Abdurahaman Shillow kushoto na anayefuatia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi Mwanaisha Ulenge
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu amehimiza umoja na mshikamano baina ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kuweza kuwatumikia vyema wananchi wa Jiji la Tanga.

Mhe Ummy ameyasema hayo leo katika kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Jiji la Tanga ambapo ameeleza kuwa uchaguzi umekwisha na wananchi wa Tanga Mjini wamewaamini kwa kuwapa ushindi mkubwa kwa mgombea Urais, Ubunge na Madiwani wa CCM katika kata zote 27 za Tanga Mjini.

Alisema baada ya uchaguzi huo kumalizika viongozi hao wana wajibu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga mjini bila kuchoka ili kuleta maendeleo yao na hatimaye kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

Mhe Ummy amempongeza Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow kwa kuaminiwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga huku akihaidi kumpa ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa Tanga ulisimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.

Akitangaza matokeo hayo Mwilapwa alimtangaza Mhe Abdurahmani Shillow ambaye ni Diwani wa Kata ya Mzingani ambaye ni mgombea Umeya wa Jiji la Tanga kwa kupata kura 26 huku nafasi ya pili ikienda kwa Mhe Said Mbaruku ambae amepata kura 11 wakati Mhe Ahmed Mwinjanga amepata kura 1 katika idadi ya wapigakura walikuwa 38.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: