MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza wakati wa
mkutano wake wa kampeni kata ya Msambweni Jijini Tanga
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akimnadi mgombea
Udiwani wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimati
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza wakati wa
mkutano wake wa kampeni kata ya Msambweni Jijini Tanga
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akifurahia jambo
wakati akiwa meza kuu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja
Mstaafu Hamisi Mkoba na kushoto mgombea Udiwani wa Kata ya Msambweni
(CCM) Godias Kimati
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kulia akicheza
sambamba na msanii wa bongofleva Shilole wakati wa mkutano huo wa
kampeni
|
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kushoto akisalimiana
na msanii wa mziki wa Bongofleva nchini Shilole kabla ya kuimba wakati
wa mkutano wake wa kampeni
|
|
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akipandisha bendera
ikiwa ni ishara ya kufungua shina la wakareketwa kwenye kata ya
Msambweni
|
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Msambweni wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Msambweni wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Msambweni wakimsikiliza Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu
Wasanii
wa mziki wa Bongofleva nchini Kassim Mganga kulia akiwa na Shilole
wakifuatilia kwa umakini mkutano wa mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga
(CCM) Ummy Mwalimu
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amesema kwamba endapo atachaguliwa
kuwa Mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha fedha za Tasaf zinawanufaisha walengo na
si wengine kama ilivyo sasa.
Ummy ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya
Msambweni katika mkutano wa kampeni wa kuomba wampe ridhaa.
Alisema kwamba katika Kata ya Msambweni anafahamu kero mojawapo inayowasumbua wao na
wana Tanga ni ni fedha za Tasaf kutowafikia walengwa na hali hii inasabishwa na
baadhi ya watendaji wetu wasio waaminifu ambao huwapatia fedha watu wasiostahili
kupewa.
“ Niwaambie jambo
hili nimeanza kulifanyia kazi tutahakikisha wakazi wa Msambweni na Tanga
nzima wanaostahili kupata fedha za Tasaf wanapata”Amesema Ummy
Mwalimu.
Aidha pia
Ummy ameahidi kutatua changamoto ya Elimu kwakusukuma maboresho ya Miundombinu
katika Shule ya Msingi Msambweni na Sekondari yake ili kuondosha kero zilizopo.
“Lakini pia
sijalisahau Daraja kutoka Chuo cha Zaharau hadi Ofisi ya Kata na kusafisha
dimbwi la Maji linalozalisha mbu katika Mtaa wa Msambweni C “Alisema
Hata
hivyo alisema kwamba atakikisha pia anaifanyia kazi changamoto ya kata hiyo
kutokuwa na Zahanati hatua inayowalazimu kwenda kwenye kata nyengine kupata huduma
hiyo.
“Kata
hii ya Msambweni haina zahanati niaminini jambo hilo nitalifanyia kazi kuhakikisha
wananchi wa hapa mnapata huduma za afya badala ya kwenda kwenye kata nyengine”Alisema
Toa Maoni Yako:
0 comments: