Na Shamimu Nyaki – WHUSM Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametangaza rasmi  kuwa kuanzia leo Julai 29, 2020 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam utaitwa Uwanja wa  Uwanja wa Benjamin Mkapa (Benjamin Mkapa Stadium) ili kuendelea kumuenzi Rais huyo wa  awamu ya Tatu.

Rais Magufuli ametoa tamko hilo katika hafla ya kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa serikali ya awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru  Dar es Salaam ambapo alisisitiza Mzee Mkapa alikuwa na mchango mkubwa katika sekta ya  michezo nchini hivyo taifa tunapaswa kumuenzi .

“Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo na alikua hapendi vitu viitwe kwa jina  lake, lakini kwakuwa kwa sasa amelala na hawezi kuniadhibu na kwakua nimepokea meseji  nyingi nimekubali na sasa natamka rasmi uwanja ule uitwe Mkapa Stadium,”Dkt.Magufuli.

Dkt.Magufuli ameongeza katika Michezo Mzee Mkapa alikuwa anapenda sana michezo ndio  maana amefanya mambo mengi sana katika sekta hiyo,vile vile alikua ni Shabiki wa Timu ya Yanga japo hakuwahi kuonyesha hadharani hivyo tunapaswa kumkumbuka na kutunza  kumbukumbu hizo.

Hata hivyo Uwanja wa Taifa Dar es Salaam (Mkapa Stadium) ni miongoni mwa viwanja  vikubwa barani Afrika ambavyo vimekidhi vigezo vyote vilivyoanishwa na Shirikisho la  Soka Duniani FIFA na una uwezo wa kuingiza mmashabiki takriban elfu sitini.

Hivi karibuni watu wengi walionyesha nia yao ya kuomba uwanja huo uitwe jina la  Mzee Mkapa kama njia ya kumuenzi Rais huyo mstaafu ambayo leo Mhe.Rais ameitimiza nia hiyo.

Pamoja Mheshimiwa Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa Mzee Mkapa katika sekta ya Sanaa napo ameacha alama kwani ndiye aliyeanzisha Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki (COSOTA)  ambayo kwa sasa ni taasisi rasmi lengo ni kuwasaidia wasanii kupata haki za kazi zao na katika sekta ya Habari ndiye muasisi wa Vitengo vya Habari na Mawasiliano katika wizara.

Naye mmoja wa wananchi na shabiki wa mpira nchini Bw.Athuman Ugassa amepongeza uamuzi  Mheshimiwa Rais Magufuli wa kuupa uwanja huo jina lake kwani uwanja huo ni alama ya  mchango wake katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: