Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru amewaongoza wadau wa haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huku akivitaka vyombo vya usimamizi wa sheria kuzingatia usawa na haki dhidi ya kesi zinazohusu vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kilele cha Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Kauli Mbiu ya “Kizazi chenye Usawa : Simama Dhidi ya Ubakaji” kimefanyika leo Desemba 10,2019 katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack.

Akizungumza, Otaru alisema ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni vyema vyombo vya usimamizi wa sheria ikijumuisha jeshi la polisi na mahakama kuzingatia haki na usawa katika maamuzi ya kesi zinazokiuka haki za Wanawake na Watoto 


Otaru alitumia fursa hiyo pia kuitaka jamii kuachana na mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili huku akitaka kuwepo kwa nguvu ya pamoja kupinga ndoa za utotoni zinazosababisha watoto kutopata haki ya elimu.

"Bado kuna changamoto ya uwepo na mila na desturi ya ndoa za utotoni pamoja na kukosekana na usawa wa umiliki mali. Ni wakati sasa jamii kuachana na mila potofu zinazochochea ndoa za utotoni pamoja na imani za kishirikina zinazokandamiza ustawi wa wanawake na watoto",alisema Otaru.

Alisema jamii inapaswa kutambua umuhimu wa kuzingatia haki za wanawake na watoto kwa kuwafichua wahalifu wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake pamoja na kuwashirikisha wanawake katika ngazi ya familia na ngazi mbalimbali za uongozi.


Otaru alisema mkoa wa Shinyanga unaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia huku akibainisha kuwa tayari mkoa umefanikiwa kuunda kamati 7 za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ngazi ya mkoa na wilaya pamoja na kamati 130 ngazi ya kata ambapo kati ya kamati 130, 51 zimepewa mafunzo na zimeanza kutekeleza majukumu yake.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la The Voice of Marginalized Society (TVMC),Mussa Jonas Ngangala alisema shirika lake limekuwa mdau mkubwa katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na tayari limeanzisha kamati 11 za MTAKUWWA ngazi ya kata katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga. 



“TVMC inaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha tunamkomboa mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili,tunahamasisha jamii iwe na umoja ili kusaidia wananchi kuondokana na ukatili wa kijinsia”,alisema Ngangala. 



"Tunaadhimisha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa lengo la kuongeza ushawishi, kubadilishana taarifa, uzoefu kujenga uwezo wa pamoja. Katika kupambana na tatizo la ukatili wa kijinsia tunawaomba wadau kuunganisha nguvu na kubuni mikakati ya kijamii ambayo italeta suluhisho la kudumu” aliongeza Ngangala.



ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack ambapo alisema zinahitajika nguvu za pamoja ili kukomesha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la The Voice of Marginalized Society (TVMC),Mussa Jonas Ngangala akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga,Mfinanga John akitoa taarifa ya jeshi la polisi kuhusu kesi za ukatili wa kijinsia wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Maafisa wa polisi Dawati la jinsia na watoto mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Mkurugenzi wa Huheso Foundation Juma Mwesigwa akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Wanafunzi wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Wadau wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Wanafunzi wakitoa burudani kwenye kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Kundi la Ngoma za Asili  maarufu Mabulo ya Jeshi linaloongozwa na Msanii Wanzingiza likitoa burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Meza kuu wakifuatilia burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Burudani ya Ngoma ya Ununguli kutoka Bugimbagu ikiendelea.


Msanii Wanzigiza kutoka Isela halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiimba wimbo maalumu wa kupinga ukatili wa kijinsia.

Wanafunzi wakiwa kwenye maaandamano kuelekea katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga ambapo kilele cha maadhimisho ya kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika Uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga leo Desemba 10,2019.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: